-->

Breaking News

Odsonne Edouard Akataa Kuichezea Haiti Kombe la Dunia 2026

Odsonne Edouard Akataa Kuichezea Haiti Kombe la Dunia 2026

Wakati wanasoka wengi wakitamani kuwakilisha timu zao za taifa kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa, hali imekuwa tofauti kwa mshambuliaji wa RC Lens, Odsonne Edouard.

Nyota huyo mwenye asili ya Haiti amezua gumzo baada ya kukataa nafasi ya kuiwakilisha timu ya taifa ya Haiti kwenye Kombe la Dunia 2026.

Edouard, ambaye ni raia wa Ufaransa lakini wazazi wake wana asili ya Haiti, alipewa nafasi ya kuitumikia Haiti baada ya taifa hilo kufuzu World Cup kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974.

Akielezea sababu ya uamuzi wake, mshambuliaji huyo amesema hajihisi kuwa na haki ya kucheza mashindano hayo makubwa kwa sababu hakushiriki safari ya kufuzu.

“Sipo tayari kuja dakika za mwisho na kunufaika na juhudi zao. Kama nitacheza, basi ni lazima nistahili,” amesema Edouard.

Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti huku mashabiki wengi wakimsifu kwa kuonyesha heshima kwa wachezaji waliopigania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Msimu huu, Edouard ameonyesha kiwango bora akiwa na RC Lens baada ya kufunga mabao 14 katika michezo 36 kwenye michuano yote.

Haiti ipo Kundi C kwenye Kombe la Dunia 2026 na itaanza kampeni zake dhidi ya Scotland Juni 14 kabla ya kucheza dhidi ya Brazil Juni 20 na Morocco Juni 25.

Uamuzi wa Edouard umeendelea kuwa moja ya habari zinazojadiliwa zaidi kwenye soka la kimataifa kuelekea World Cup 2026.

Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za World Cup 2026, soka la Ulaya na breaking news za michezo duniani.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.