Nicki Minaj Aibua Gumzo Baada ya Kumuunga Mkono Trump
Nicki Minaj Afunguka Sababu ya Kumuunga Mkono Donald Trump Hadharani
Nicki Minaj ameweka wazi sababu iliyomfanya kumuunga mkono Donald Trump hadharani, akisema wasanii wengi wana mawazo kama yake lakini wanaogopa kuyasema wazi.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, rapa huyo maarufu kutoka Marekani alisema aliamua kuzungumza wazi kuhusu msimamo wake wa kisiasa ili kuwapa wengine ujasiri wa kueleza wanachokiamini bila hofu ya kukosolewa.
Nicki Minaj alieleza kuwa kwa muda mrefu alikuwa akiunga mkono Trump, lakini alisita kuweka wazi msimamo huo kutokana na mazingira ya tasnia ya burudani ambayo kwa kiasi kikubwa inaunga mkono chama cha Democrats.
Msanii huyo pia alisema baadhi ya watu maarufu wanaunga mkono Trump kwa siri, lakini wanaepuka kusema hadharani kwa kuhofia kupoteza mashabiki au kukosolewa kwenye mitandao ya kijamii.
Kauli za Nicki Minaj zimezua mjadala mkubwa mtandaoni, huku mashabiki na wachambuzi wa burudani wakitoa maoni tofauti kuhusu msimamo wake wa kisiasa.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari za burudani, mastaa wa kimataifa, na matukio yanayotrend duniani.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.