Mo Dewji Akutana na Benchi la Ufundi na Wachezaji wa Simba
Mo Dewji Akutana na Wachezaji wa Simba SC Kuwapa Hamasa
Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji, amekutana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwapa hamasa kuelekea michezo ya mwisho ya msimu wa 2025/26.
Katika kikao hicho, Mo Dewji aliwataka wachezaji kuendelea kujituma na kupambana kwa nguvu zote ili kuhakikisha Simba SC inamaliza msimu kwa mafanikio makubwa.
Pia alisisitiza umuhimu wa mshikamano, nidhamu na kujitolea ndani na nje ya uwanja, akieleza kuwa ana imani kubwa na kikosi hicho pamoja na benchi la ufundi.
Kwa upande wao, wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi walimshukuru Mo Dewji kwa sapoti na motisha anayoendelea kutoa, wakiahidi kupambana kwa nguvu zote ili kufikia malengo ya klabu.
Simba SC wanaendelea na maandalizi ya michezo yao ya mwisho ya msimu huku mashabiki wakiwa na matumaini makubwa ya kuona timu yao ikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za Simba SC, Yanga SC, NBC Premier League na soka la Tanzania kwa ujumla.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.