Mfahamu Princess Norodom Jenna: Binti Mfalme Aliyetikisa Muziki na Uigizaji Asia
Mfahamu Princess Norodom Jenna: Binti Mfalme Aliyetikisa Muziki na Uigizaji Asia
Princess Norodom Jenna ni miongoni mwa watoto wa kifalme wanaofuatiliwa zaidi barani Asia kutokana na kipaji chake katika muziki, uigizaji na uwezo wake wa kuzungumza lugha mbalimbali.
Jenna alizaliwa Machi 11, 2012 jijini Paris, Ufaransa na ni binti wa Princess Norodom Bophary kutoka familia ya kifalme ya Cambodia, akiwa pia kitukuu cha marehemu Mfalme Norodom Sihanouk.
Baada ya kuhamia Cambodia akiwa na umri mdogo, alisomea na kuendeleza kipaji chake cha sanaa katika Music Arts School iliyopo Phnom Penh.
Mojawapo ya sifa zinazomtofautisha ni uwezo wa kuzungumza lugha tano ambazo ni Khmer, Kifaransa, Kiingereza, Kithai na Kichina, jambo lililomsaidia kupata mashabiki duniani.
Tofauti na matarajio ya maisha ya kifalme ya kuwa mbali na mitandao ya kijamii, Jenna amekuwa akitumia majukwaa kama YouTube, TikTok na mengine kuonyesha vipaji vyake.
Ameingia rasmi kwenye muziki kupitia nyimbo za cover na K-Pop, akivutia mashabiki wengi kutokana na uchezaji wake unaofananishwa na nyota wa BLACKPINK, Lisa.
Baadaye alitoa nyimbo zake kama “Falling” na “Truth or Game”, ambazo ziliongeza umaarufu wake na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii chipukizi wanaofuatiliwa Asia.
Pia Jenna ni mwigizaji ambapo alianza akiwa na umri wa miaka sita kupitia televisheni ya taifa ya Cambodia.
Mwaka 2024 alishinda tuzo ya Best Newcomer Actress katika Cambodia-Asia Film Festival kutokana na uhusika wake kwenye filamu ya kutisha “The Night Curse of Reatrei.”
Kutokana na ushawishi wake, Jenna amekuwa balozi wa kampuni mbalimbali kubwa za kimataifa na pia ameendelea kutambulisha utamaduni wa Cambodia duniani.
Mwezi Aprili 2026 alitunukiwa hadhi ya kifalme ya “Her Royal Highness” ikiwa ni kutambua mchango wake katika sanaa na utamaduni.
Kwa sasa Jenna anaendelea kuonekana kama moja ya nyota wachanga wa kifalme wenye ushawishi mkubwa zaidi Asia na duniani kwa ujumla.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari za burudani, mastaa na hadithi za watu maarufu duniani.



No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.