Makonda Afunguka Sababu ya Rio Ferdinand Kutopost Kuhusu Ziara ya Tanzania
Makonda Afunguka Sababu ya Rio Ferdinand Kutopost Kuhusu Ziara ya Tanzania
Paul Makonda amesema alimwomba mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand, kutopost kwa sasa kuhusu uwepo wake nchini Tanzania.
Makonda amesema jambo muhimu zaidi kwenye ziara hiyo ni maendeleo ya vijana pamoja na kuinua vipaji vya michezo nchini badala ya kujadili mambo ya mitandaoni.
Akizungumza na waandishi wa habari Mei 22, 2026 jijini Dar es Salaam, Makonda alisema kumekuwa na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kwanini Rio Ferdinand hajapost kuhusu ziara yake nchini Tanzania.
“Wakati mwingine tunapenda kubeza mambo lakini hatujui nguvu kubwa inayofanywa na viongozi wetu kufanikisha hayo mambo. Ajenda kubwa ilikuwa ni kwanini Rio hajapost kwenye akaunti yake kuwa yupo Tanzania,” alisema Makonda.
Aidha, amesema baadhi ya watu wamekuwa wakijikita zaidi kwenye mijadala ya mtandaoni badala ya kuangalia manufaa ya muda mrefu yanayoweza kupatikana kupitia ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya michezo na maendeleo ya vijana.
“Tunapenda kujadili mambo kwa kuyaona bila kuyajua na mwisho tunaamini tunajua kila kitu. Ulishawahi kufikiria mtu yupo anaongelea mema juu ya nchi yako, namna Serikali inavyopiga hatua, halafu wewe badala ya kuchukua ile content uipeleke duniani unataka yeye ndio apost?” alisema Makonda.
Ziara ya Rio Ferdinand nchini Tanzania imeendelea kuvuta hisia za wananchi na wadau wa michezo huku wengi wakiamini inaweza kufungua fursa mpya kwa vijana wenye vipaji vya soka na michezo mingine.
Rio Ferdinand ni mmoja wa mastaa wakubwa wa soka duniani aliyewahi kung’ara akiwa na Manchester United pamoja na timu ya taifa ya England.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za michezo, mastaa wa soka na maendeleo ya vijana Tanzania.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.