Mourinho Aelekea Bernabéu Tena Baada ya Miaka 13
José Mourinho Karibu Kurejea Real Madrid Kama Kocha Mkuu
José Mourinho anaripotiwa kuwa karibu kurejea tena kuinoa Real Madrid baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya pande zote mbili kufikia hatua za mwisho.
Ripoti kutoka vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya zinaeleza kuwa Mourinho amepokelewa vyema ndani ya uongozi wa klabu hiyo kutokana na uzoefu wake na mafanikio aliyowahi kuyapata katika kipindi chake cha kwanza Santiago Bernabéu.
Mourinho aliwahi kuinoa Real Madrid kati ya mwaka 2010 hadi 2013, ambapo alifanikiwa kushinda mataji ya La Liga, Copa del Rey na Super Cup ya Uhispania, huku akiweka msingi wa ushindani mkubwa dhidi ya Barcelona.
Kwa mujibu wa taarifa, makubaliano mapya yanaweza kuwa ya miaka miwili, na tangazo rasmi linatarajiwa baada ya kukamilika kwa taratibu za mwisho za klabu.
Hata hivyo, bado hakuna uthibitisho rasmi kutoka Real Madrid au Mourinho mwenyewe, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona kama “The Special One” atarudi Bernabéu.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari za soka la Ulaya, usajili na taarifa rasmi kutoka klabu kubwa duniani.
```0
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.