José Mourinho Atarejea Real Madrid kwa Mkataba wa Miaka Miwili
Here We Go! José Mourinho Arejea Real Madrid Baada ya Miaka 13
José Mourinho anatarajiwa kurejea kuinoa Real Madrid baada ya mwandishi maarufu wa usajili Fabrizio Romano kutumia kauli yake ya “Here We Go!” kuthibitisha kuwa makubaliano yamefikiwa.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mourinho amekubaliana kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Hispania, akirejea Santiago Bernabéu kwa mara ya pili baada ya kuondoka mwaka 2013.
Kocha huyo wa Ureno, maarufu kama “The Special One”, aliwahi kuifundisha Real Madrid kati ya mwaka 2010 na 2013 na kushinda mataji ya La Liga, Copa del Rey na Supercopa de España.
Uongozi wa Real Madrid unaamini uzoefu wa Mourinho unaweza kuirejesha timu kwenye kiwango cha ushindani wa juu baada ya msimu mgumu wa 2025/26.
Mashabiki wa Real Madrid wamepokea habari hiyo kwa hisia tofauti, huku wengi wakisubiri tangazo rasmi kutoka klabu hiyo.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za usajili, tetesi za Fabrizio Romano na soka la Ulaya.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.