Joao Pedro Aota Kujiunga na Barcelona, Chelsea Yataka Zaidi ya Euro Milioni 100
Joao Pedro Aota Kujiunga na Barcelona, Chelsea Yataka Zaidi ya Euro Milioni 100
Mshambuliaji wa Chelsea, Joao Pedro, anaripotiwa kuwa na ndoto ya kujiunga na Barcelona, klabu ambayo ameivutiwa nayo tangu utotoni kutokana na mafanikio ya nyota wa Brazil kama Ronaldinho, Neymar na Raphinha.
Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Joao Pedro ana mapenzi makubwa na Barcelona na angependa kupata nafasi ya kuvaa jezi ya klabu hiyo ya kihistoria ya Hispania.
Hata hivyo, Chelsea haitakuwa tayari kumwachia kirahisi. Klabu hiyo ya London ilitumia takribani euro milioni 65 kumsajili mwezi Julai mwaka jana, na kwa sasa anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi ndani ya kikosi.
Vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vinaeleza kuwa itakuwa vigumu kwa Chelsea kukubali kumuachia kwa ada ya chini ya euro milioni 100, hasa kutokana na kutokuwepo kwa kipengele cha release clause kwenye mkataba wake.
Inaelezwa pia kuwa Joao Pedro anatamani kucheza UEFA Champions League msimu ujao, jambo ambalo linaweza kuwa changamoto iwapo Chelsea haitafanikiwa kufuzu.
Barcelona ilifanya mawasiliano ya awali na upande wa mchezaji mwezi Aprili ili kufahamu msimamo wake, lakini hadi sasa hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa kwa Chelsea.
Kwa sasa, Joao Pedro ameweka nguvu zake kwenye mashindano ya FA Cup na pia kuhakikisha anapata nafasi katika kikosi cha Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026.
Mara tu msimu wa Chelsea utakapomalizika, mustakabali wa mshambuliaji huyo utaanza kujadiliwa kwa kina huku Barcelona ikisubiri kuona kama itaweza kuanzisha mazungumzo rasmi.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.