Inter Miami Yakaribia Kumsajili Casemiro, Makubaliano Yakaribia Kukamilika
Inter Miami Yakaribia Kumsajili Casemiro, Makubaliano Yakaribia Kukamilika
Inter Miami inatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo wa Manchester United, Casemiro, kuelekea dirisha lijalo la usajili.
Kulingana na ripoti kutoka kwa mwandishi wa masuala ya usajili Ben Jacobs, makubaliano ya awali kati ya pande hizo mbili yako karibu kukamilika huku mazungumzo yakiendelea vizuri.
Casemiro ambaye amewahi kung’ara akiwa Real Madrid na Manchester United, anaweza kuwa nyota mwingine mkubwa kuhamia ligi ya Marekani MLS.
Inter Miami imeendelea kuvutia mastaa wakubwa wa soka duniani tangu kuwasili kwa Lionel Messi, huku klabu hiyo ikisaka kuongeza uzoefu mkubwa kwenye kikosi chake.
Iwapo dili hilo litakamilika, Casemiro ataungana na baadhi ya nyota wakubwa wanaocheza ndani ya MLS na kuongeza ushindani mkubwa kwenye ligi hiyo.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za usajili, Manchester United na soka la kimataifa.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.