-->

Breaking News

Instagram “Great Purge 2026”: Mastaa Duniani Wapoteza Mamilioni ya Followers

Instagram “Great Purge 2026”: Mastaa Duniani Wapoteza Mamilioni ya Followers

Mtandao wa Instagram umeibua mjadala mkubwa duniani baada ya kuripotiwa kufanya usafi mkubwa wa akaunti fake, spam pamoja na akaunti zisizo na shughuli kupitia mfumo wa AI wa kampuni ya Meta.

Hatua hiyo ambayo watumiaji wengi wameipa jina la “Great Purge of 2026” imesababisha mastaa mbalimbali duniani kupoteza mamilioni ya followers ndani ya muda mfupi.

Mastaa Wakubwa Walioathirika

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa mitandaoni, baadhi ya mastaa waliopoteza followers ni pamoja na:

  • Cristiano Ronaldo
  • Lionel Messi
  • Selena Gomez
  • Taylor Swift
  • Kim Kardashian
  • Beyoncé
  • Ariana Grande
  • Dwayne Johnson

Ronaldo Na Messi Waongoza Kwa Kupoteza Followers

Ripoti zinaonyesha kuwa Cristiano Ronaldo ameripotiwa kupoteza zaidi ya milioni 6.6 ya followers, huku Lionel Messi akipoteza karibu milioni 4.8, ikiwa ni sehemu ya usafi huo mkubwa wa akaunti zisizo halisi.


Lengo La Meta Ni Kupambana Na Akaunti Fake

Meta inadaiwa kulenga kupunguza akaunti bot, spam na huduma za kuongeza followers kwa njia zisizo halali ili kuboresha uhalisia wa engagement kwenye platform hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya watumiaji wanaamini kuwa baadhi ya akaunti halisi pia zinaweza kuathirika kutokana na mfumo wa AI kufanya usafi kwa kiwango kikubwa kwa wakati mmoja.

Watumiaji Wadogo Pia Waathirika

Mbali na mastaa wakubwa, creators wadogo na wa kati nao wameripoti kupoteza kati ya asilimia 2 hadi 5 ya followers wao katika muda mfupi, hali inayoendelea kuibua mjadala mkubwa mitandaoni.

Mjadala kuhusu “Instagram Great Purge 2026” unaendelea kushika kasi huku watumiaji wakisubiri taarifa rasmi kutoka Meta.

🔴 Cristiano Ronaldo
http://instagram.com/cristiano
Previous : 673,307,250
Current : 666,695,107
Change : -6,612,143 (lost)

🔴Lionel Messi
http://instagram.com/leomessi
Previous : 512,532,381
Current : 507,722,140
Change : -4,810,241 (lost)

🔴Selena Gomez
http://instagram.com/selenagomez
Previous : 414,324,851
Current : 408,836,859
Change : -5,487,992 (lost)

🔴 Taylor Swift
http://instagram.com/taylorswift
Previous : 279,993,327
Current : 275,827,600
Change : -4,165,727 (lost)

🔴 Kim Kardashian
http://instagram.com/kimkardashian
Previous : 352,635,698
Current : 347,507,844
Change : -5,127,854 (lost)

🔴 Jennifer Lopez
http://instagram.com/jlo
Previous : 245,702,759
Current : 242,271,800
Change : -3,430,959

🔴 Beyonce
http://instagram.com/beyonce
Previous : 307,211,182
Current : 302,761,202
Change : -4,449,980 (lost)

🔴 Ariana Grande
http://instagram.com/arianagrande
Previous : 371,415,576
Current : 365,838,792
Change : -5,576,784 (lost)

🔴 Priyanka Chopra
http://instagram.com/priyankachopra
Previous : 94,558,158
Current : 93,413,034
Change : -1,145,124 (lost)

🔴Katy Perry
http://instagram.com/katyperry
Previous : 200,574,213
Current : 197,583,900
Change : -2,990,313 (lost)

🔴Zendaya
http://instagram.com/zendaya
Previous : 177,281,901
Current : 175,254,149
Change : -2,027,752 (lost)

🔴 Dwayne Johnson
http://instagram.com/therock
Previous : 390,068,666
Current : 385,173,978
Change : -4,894,688 (lost)

#Instagram, #Meta, #Social Media, #Technology, #Celebrities, #Trending News, #AI

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.