-->

Breaking News

Diamond Platnumz Aongoza YouTube Kenya Akivuka Watazamaji Milioni 160 kwa Mwaka Mmoja


Diamond Platnumz Aongoza YouTube Kenya Akivuka Watazamaji Milioni 160

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameendelea kuonesha ukubwa wake baada ya kushika nafasi ya kwanza kama msanii wa Afrika Mashariki aliyeangaliwa zaidi nchini Kenya kupitia mtandao wa YouTube.

Rekodi Ya Watazamaji Milioni 160

Kulingana na takwimu zilizotolewa kupitia media mbalimbali, Diamond Platnumz amefikisha zaidi ya watazamaji milioni 160 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, akijipatia nafasi ya juu katika streaming za muziki nchini Kenya.

Wasanii Wengine Kumi Bora YouTube Kenya

  • Mbosso – milioni 147
  • Harmonize – milioni 141
  • Marioo – milioni 132
  • Vybz Kartel – milioni 120
  • Prince Indah – milioni 117
  • Zuchu – milioni 111
  • Toxic Lyrikali – milioni 95.9
  • Rayvanny – milioni 94.2
  • Bien – milioni 87.2

Ushindani Wa Muziki Afrika Mashariki

Takwimu hizi zinaonyesha ukuaji mkubwa wa muziki wa Afrika Mashariki kidigitali, huku Diamond Platnumz akiendelea kuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa zaidi katika soko la muziki la kikanda na kimataifa.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.