Deco Akutana na Wakala wa Joao Pedro Katika Mpango wa Barcelona
Barcelona Wamuanza Joao Pedro, Deco Akutana na Wakala wa Straika wa Chelsea
Barcelona wameongeza juhudi za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Joao Pedro, baada ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Deco, kuripotiwa kukutana na wakala wa mchezaji huyo jijini London.
Joao Pedro amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu na ameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao pamoja na kucheza katika nafasi tofauti za ushambuliaji.
Barcelona wanatajwa kumtazama nyota huyo wa Brazil kama mmoja wa wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi ya Robert Lewandowski katika siku zijazo.
Hata hivyo, Chelsea hawana nia ya kumuachia kirahisi mchezaji huyo ambaye amekuwa sehemu muhimu ya kikosi chao tangu alipojiunga na klabu hiyo.
Ripoti zinaeleza kuwa mazungumzo bado yapo katika hatua za awali, na hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa kati ya pande zote mbili.
Endelea kufuatilia IddyNation kwa tetesi zote za usajili, habari za soka la Ulaya, na taarifa rasmi kutoka klabu kubwa duniani.
.jpeg)
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.