Andres Iniesta Kuwa Kocha Mkuu wa Gulf United Dubai
Andres Iniesta Kuanza Kazi Yake ya Kwanza ya Ukocha Dubai
Nguli wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Andres Iniesta, anatarajiwa kuanza rasmi kazi yake ya kwanza ya ukocha baada ya kufikia makubaliano na klabu ya Gulf United ya Dubai. 1
Mwandishi maarufu wa habari za usajili duniani, Fabrizio Romano, ameripoti kuwa kila kitu tayari kimekubaliwa huku Iniesta akisubiri kusaini rasmi mkataba wake mpya. 2
Iniesta atakuwa kocha mkuu wa Gulf United FC inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza nchini Falme za Kiarabu (UAE), huku hii ikiwa hatua mpya baada ya kustaafu soka mwaka 2024. 3
Baada ya kutundika daruga, Iniesta alianza kuchukua mafunzo ya ukocha akiwa Asia huku akionesha nia ya kuendelea kubaki kwenye dunia ya soka kupitia benchi la ufundi. 4
Katika mahojiano yake ya awali, Iniesta aliwahi kusema anatamani siku moja kurejea Barcelona akiwa kocha baada ya kumaliza safari yake ya mafanikio kama mchezaji ndani ya klabu hiyo. 5
Iniesta anatajwa kuwa mmoja wa viungo bora kuwahi kutokea duniani baada ya kushinda mataji mengi akiwa Barcelona pamoja na Hispania ikiwemo Kombe la Dunia 2010 na UEFA Euro. 6
Safari yake mpya ya ukocha imeibua hisia kubwa kwa mashabiki wa soka duniani huku wengi wakiamini uwezo wake mkubwa wa kuelewa mchezo unaweza kumfanya kuwa kocha bora siku zijazo.
Gulf United ni klabu yenye makazi yake Dubai ambayo imekuwa ikiwekeza zaidi kwenye maendeleo ya vijana pamoja na kukuza soka nchini UAE. 7
Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za soka duniani, makocha, usajili na mastaa wa football.
```8
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.