-->

Breaking News

Video za AI zinavyotikisa mitandaoni

 Video za AI zinavyotikisa mitandaoni

Wakati dunia ikiendelea kushuhudia mabadiliko makubwa ya teknolojia. Imeibuka aina mpya ya burudani inayotikisa mitandao ya kijamii na kuvutia mamilioni ya watazamaji.

Ni kuhusu video za stori fupi zijulikanazo kama ‘AI fruit dramas’ ambazo hutengenezwa kwa kutumia akili bandia (AI). Wahusika wanaotumika ni matunda kama ndizi, tufaha, machungwa na matunda mengine yakibadilishwa kuwa wahusika katika filamu fupi za stori.



Video hizo zimekuwa zikionekana kwenye mitandao kama TikTok na Instagram, huku baadhi zikipata mamilioni ya watazamaji ndani ya muda mfupi. Watazamaji wanakiri kuwa video hizi zimekuwa sehemu ya maisha yao, wakizitazama kwa nia ya kujifariji hasa nyakati za usiku, na baadhi zikitoa mafunzo ya maisha ya kila siku.

Video hizo hazitengenezwi na watu wa kawaida bali hutengenezwa kwa kutumia programu za AI zinazoweza kutengeneza picha, sauti na hata simulizi kamili, ambapo mtumiaji anaandika wazo ama stori yake kisha teknolojia hiyo inatengeneza kila kitu kuanzia mwonekano wa muhusika hadi sauti yake.

Aidha mchambuzi wa masuala ya mitandao ya kijamii, Anna Rawhiti-Connell, anasema kuwa wapenzi wa mitandao ya kijamii sasa wamebadili mwelekeo kwani zamani walikuwa wakivutiwa sana na maudhui ya kawaida ila kwa sasa wanavutiwa zaidi na vitu vya kushangaza na visivyotabirika.

Ingawa video hizi zinaonekana kama burudani za kuchekesha na kupotezea muda, ukweli ni kwamba zina nguvu kubwa sana kwa sababu, zinawavutia watu wengi kwa haraka lakini pia zinawafanya watu wazungumzie (kujadili).

Hata hivyo, si kila mtu anavutiwa na stori hizo waadhi ya wafuatiliaji wanaeleza kuwa zipo baadhi ya video zimebeba maudhui yasiofaa hususani kwa watoto huku wakitaka zizuiliwe mara moja kwa ajili ya usalama wa watoto.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.