Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Newcastle inamfukuzia Ugarte Man Utd(Habari za michezo 2026)
Newcastle United inataka kuimarisha safu yake kati msimu huu na wanapania kumsajili kiungo wa Manchester United Manuel Ugarte, 25,(Football Insider)
Tottenham Hotspur na West Ham United zina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Marc Casado, 22. (Tuttomercato - kwa Kiitaliano).
Liverpool na Chelsea wako tayari kupigana vikumbo kwa mshambuliaji wa Bournemouth Eli Junior Kroupi, 19, huku Cherries wakiwa tayari kukubali ofa ya pauni milioni 60. (Caught Offside)
Coventry City inataka uhamisho wa mkopo wa mlinda lango wa Brighton Carl Rushworth, 24, kuwa wa kudumu msimu wa joto lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Leeds United. (Team Talk)
( kwa Habari za michezo ,wasanii na nyimbo mpya kila siku tembelea https://www.iddynation.site )

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.