Tetesi za soka Ulaya: Bayern, Arsenal 'zatoana roho' kwa Anthony Gordon
Chanzo cha picha,
Bayern Munich wameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Newcastle United na England, Anthony Gordon, mwenye miaka 25, ambaye pia anafuatiliwa na Arsenal (Caughtoffside).
Manchester United wanatarajia kutumia uhusiano ulioko ndani ya kikosi cha England kuwazidi kete Manchester City katika mbio za kumsajili kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, mwenye miaka 23 (Teamtalk).
Liverpool wanamfuatilia winga wa Brighton & Hove Albion na Gambia, Yankuba Minteh, mwenye miaka 21, aliyewahi kufanya kazi chini ya Arne Slot huko Feyenoord, kama mbadala wa mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, anayeondoka mwishoni mwa msimu (Mirror).

Arsenal na Manchester City wameungana na Aston Villa katika mbio za kumsajili beki wa Real Betis, Oscar Mingueza, mwenye miaka 26 (Teamtalk).
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.