-->

Breaking News

OPPO yazindua mwavuli janja unaofanya kazi kama simu

 OPPO yazindua mwavuli janja unaofanya kazi kama simu

Kampuni ya teknolojia ya simu na vifaa mbalimbali kutoka China, OPPO, imezindua mwavuli janja uitwao OPPO Find U, ambao umebuniwa kufanya kazi kama simu, ukimwezesha mtumiaji kuperuzi na kutumia huduma za kidijitali kama kawaida hata akiwa kwenye mvua.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, bidhaa hiyo mpya si mwavuli wa kawaida bali ni mapinduzi makubwa katika teknolojia ya vifaa vinavyotumika kila siku. OPPO imesema imetumia teknolojia ya simu zinazokunjika na kuubadilisha kuwa kifaa kinachoweza kutumika nje, hata wakati wa mvua.



Katika uzinduzi huo, OPPO ilieleza kuwa mwavuli huo umejengwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya bawaba inayojulikana kama Find N6 Flexion Hinge, ambayo imefanyiwa majaribio Zaidi ya mara 600,000 ili kuhakikisha uimara na ubora wake unakuwa wa muda mrefu.

Mbali na uimara wake, mwavuli huo umewekewa ubunifu wa hali ya juu unaoruhusu mtumiaji kubadilisha rangi (canopy) kwa kubonyeza tu mpini, ili kuendana na mavazi au mtindo anaouhitaji.

Katika hatua nyingine, OPPO imeongeza vipengele vya kisasa vinavyoufanya Find U kuwa zaidi ya mwavuli:

Moja ya sifa kuu ni uwepo wa skrini ya 4K inayomwezesha mtumiaji kuangalia video, kuperuzi mitandao ya kijamii au hata kufanya mawasiliano ya video bila kuathiriwa na mvua.

Aidha, mpini wa mwavuli huo umewekewa kamera yenye uwezo sawa na ile ya simu za kisasa za kampuni hiyo, hivyo kumruhusu mtumiaji kupiga picha hata wakati wa mvua bila kuharibu kifaa.

Kwa upande wa usalama, mwamvuli huo umewekewa mfumo wa alama za vidole (fingerprint), ambapo ni mmiliki pekee anayeweza kuufungua. Pia kuna mfumo wa “Solar Mode” unaoruhusu mwavuli huo kukusanya nishati ya jua na kuutumia kama power bank ya kuchaji vifaa vingine.

Katika kuhakikisha matumizi rahisi zaidi, OPPO imeweka teknolojia ya kukausha maji kwa mtetemo wa kasi ya juu (60,000Hz), pamoja na mfumo wa akili bandia unaoweza kukabiliana na upepo mkali.

Akizungumzia ubunifu huo, mmoja wa kiongozi, Dkt. Rainn E. Daye, amesema kifaa hicho kinawakilisha hatua mpya katika uhandisi wa teknolojia ya mazingira.

“Tumefanikiwa kuhamisha ubora wa skrini ya Find N6 kwenye umbo la mwavuli, jambo lililohitaji ubunifu mkubwa wa kisayansi. Hii si tena kinga ya mvua tu, bali ni uzoefu kamili wa kidijitali ukiwa njiani,” alisema.

Kwa mujibu wa OPPO, mwavuli huo wa kisasa unatarajiwa kuanza kupatikana rasmi kuanzia Aprili 31, 2026 huku kampuni hiyo ikipanga kuanza kuutambulisha kupitia matukio maalum ya uzinduzi katika jiji la London na maeneo mengine duniani.


Hata hivyo, kampuni hiyo imesema taarifa kamili kuhusu bei na upatikanaji katika masoko mbalimbali zitatolewa baadaye.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.