-->

Breaking News

Mfahamu Mehmet aliyenyuma ya filamu za Uturuki

 Mfahamu Mehmet aliyenyuma ya filamu za Uturuki

Sekta ya filamu nchini Uturuki imekuwa sehemu muhimu ya kutangaza historia na utamaduni wa watu wake.

Yakitajwa majina ya watengeneza tamthilia za kihistoria, Mehmet Bozdağ haliwezi kukosekana. Hii ni kutokana na kuupiga mwingi katika upande huo.

Mehmet Bozdağ alizaliwa mwaka 1983 katika mji wa Kayseri, nchini Turkey. Toka alipokuwa mtoto alipendelea sana kufuatilia historia na simulizi za zamani jambo ambalo lilimsukuma kwenda kusomea tasnia hiyo.



Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi na sekondari jijini Kayseri. Bozdağ aliendelea na masomo ya juu katika chuo cha Sakarya. Ambapo alisomea Historia kwa shahada ya kwanza, kisha akapata shahada ya uzamili (Master’s) katika Sosholojia.

Akiwa na mapenzi makubwa ya historia, alianza safari yake ya kitaaluma mwaka 2009 kwa kuandika makala za kihistoria kama Son Rüya na Kardeş Şehirler. Baadaye alihusika katika utayarishaji wa simulizi kuhusu mshairi wa Kisufi wa karne ya 13, Yunus Emre. Hatua iliyodhihirisha wazi mwelekeo wake wa kuifufua historia kupitia sanaa.

Hata hivyo jina lake lilianza kutambulika baada ya kupata mafanikio makubwa katika tamthilia ya Diriliş: Ertuğrul, filamu ambayo aliiandika na kuitayarisha mwenyewe. Tamthilia hiyo ilianza mwaka 2014 na kumalizika mwaka 2019 ikiwa na jumla ya vipande 150, kazi ambayo ilifanikiwa kuvuka mipaka na kutazamwa Zaidi ya nchi 70 huku ikiwavutia mamilioni ya watazamaji.

Aidha baada ya kupata mafanikio hayo aliamua kuanzisha kampuni ya uzalishaji wa filamu na tamthilia ijulikanayo kama ‘Bozdağ Film’. Kampuni ambayo imejikita katika kuandaa tamthilia zinazohusu historia ya Dola ya Ottoman, mashujaa wa Uturuki, na simulizi zenye msingi wa tamaduni na maadili ya kale.

Mbali na kampuni hiyo ameanzisha shule maalumu ya waigizaji kujifunza mbinu za kupigana, kupanda farasi, na kuishi maisha ya zamani.

Kuhusu seti ya kuigizia iliyogeuka kivutio Uturuki

Mafikirio na mafanikio yake hayakuishia kwenye kutengeneza filamu bora tuu. Pia amefanya uwekezaji mkubwa ambao umegeuka kuwa kivutio cha kipekee nchini Uturuki.

Kupitia kampuni yake ya Bozdağ Film, alianzisha kambi maalum ya uzalishaji wa filamu za kihistoria ijulikanayo kama ‘Bozdağ Film Plateau’ iliopo Riva (Beykoz district), nje kidogo ya Istanbul, eneo lililojengwa kwa uhalisia mkubwa kuakisi maisha ya enzi za Dola ya Ottoman.

Ndani ya kambi hiyo, kuna vijiji vya kale, masoko, majumba ya kifalme pamoja na maeneo ya vita, yote yakiwa yameundwa kwa ustadi mkubwa ili kuwapa waigizaji mazingira halisi ya kuishi na kuigiza.



Tofauti na seti za kawaida zinazojengwa kwa muda mfupi. Kambi hii imekuwa ya kudumu ambapo kwasasa watu kutoka mataifa mbalimbali pamoja na viongozi wakubwa duniani hutembelea eneo hilo kwa ajili ya kufanya utalii.



Tuzo alizowahi kupata

Kupitia filamu hizo za kihistoria Mehmet Bozdağ amefanikiwa kupata tuzo kubwa ndani na nje ya Uturuki tuzo za ubora wa uigizaji, skripti na utayarishaji.


Miongoni mwa tuzo hizo ni Golden Palm Awards kwa Mwandishi Bora, Turkey Youth Awards kama Mtayarishaji wa Mwaka, KTÜ Media Awards skripti bora pamoja na Golden Butterfly Awards kama Tamthilia Bora ya TV.

Kwa takribani miaka 10 sasa katika utengenezaji wa filamu za kihistoria Bozdağ amefanikiwa kuachia filamu mbalimbali ikiwemo Diriliş: Ertuğrul (2014–2019), mwendelezo wake Kuruluş: Osman (2025–sasa), pamoja na tamthilia kama Yunus Emre: The Journey of Love (2015–2016), Mehmetçik: Kut'ül Amare (2018) na Mendirman Jaloliddin (2021

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.