-->

Breaking News

Mbinu za kutengeneza filamu zitazouzika kimataifa

 Mbinu za kutengeneza filamu zitazouzika kimataifa

Katika ulimwengu wa filamu, ambao kila sekunde ya picha na sauti inaweza kuamua hatima ya hadithi. Uandishi mzuri pekee hauwezi kuipa filamu thamani ya kutosha badala yake umakini katika kila hatua unahitaji katika vipengele vyote vya uzalishaji.

Kutokana na baadhi ya waandaaji wa filamu hizo kutozingatia hatua za uandaaji wa filamu imekuwa sababu ya soko hilo kudidimia na wakati mwingine kukosa nafasi ya kuoneshwa katika vipindi mbalimbali vya runinga ndani na nje ya nchi. Ambavyo kwa sasa biashara ya kazi hizo imehamia huko.

Akitolea ufafanuzi wa namna ya kutengeneza filamu zenye ubora zinazoweza kuuza kimataifa na kwenye vipindi vya runinga nchini Ilham Rashid Mjumbe Kamati ya Maudhui kutoka Azam Media, ambao ni miongoni mwa wanunuaji wa kazi hizo za sanaa alieleza licha ya hadithi za filamu kuweza kuandikwa kutokana na mambo yanayozunguka jamii pia zinaweza kuandikwa kutokana na mambo ya kufikirika

“ Siyo lazima kuwa na mambo yaliyopo kwenye jamii kuna vitu vya kusadikika ambavyo vinaweza kuandikiwa filamu, hakuna kitu kizuri kama kutengeneza stori ambayo wewe mwenyewe unaijua. Mazingira yako yawe vipi, watu wako wawe vipi, na hakuna mtu atakayeweza kukubishia kwa sababu ni dunia yako mwenyewe ukiangalia vitu vya kufikirika na visivyo vya kufikirika unaweza kutengenea filamu nzuri na ikauza.

“Nashauri kwenye filamu za Bongo tujaribu kufanya tafiti, tusome, tuwe na uthubutu tunaweza. Kuna movie zimetengenezwa tangu mwaka 1999 lakini hadi sasa zinatazamwa,”alisema

Akikazia hilo Mhadhiri Idara ya Sanaa na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Issa Mbura alisema biashara yoyote ya filamu ili ifanye vizuri haihitaji kufanyika katika mazingira ya kila siku.

“Biashara zote za mafanikio katika filamu hawazalishi uhalisia katika maisha ya kila siku kwa lugha nyingine tunaweza kusema watu wanatazama filamu ili waukimbie uhalisia kwa hiyo kama ukiona unaandika filamu yako ikiakisi uhalisia tayari umekosea.

“Hata hizo ambazo tunazitazama jaribu kufikiria kuna mnyama kama Godzilla au King Kong kuna mtu ana uwezo wa kimwili kama Spider Man au Bat Man na ndiyo filamu zenye mafanikio lakini sisi tunatakiwa kufikiri nje ya box uthubutu ndiyo unakosekana,”alisema

Alisema waandaaji wa filamu wakitoka kwenye kufikilia uhalisia zaidi kazi za filamu nchini zitaenda mbali.



“Sisi tukiwatoa watu katika kufikiria kwenye kuongea zaidi na tukawaweka kwenye kufanya wajikite kwenye kitu ambacho siyo kila mtu anaweza kufanya lazima muhusika aongezewe sifa hicho kitu kitatukuza moja kwa moja,”alisema

Hata hivyo wataalamu hao wanasisitiza kamera nzuri ya kurekodia ni muhimu kuendana na uhalisia wa filamu. Baada ya kumaliza kurekodi filamu ni muhimu kuzingatia uchaguzi wa rangi na sauti.

Kingine kinachosisitizwa ni umuhimu wa kuzingatia muziki ambao unaendana na maudhui. Kwani upo mwingine ukiweka unapoteza kabisa maana ya hadithi bila kusahau rangi ni muhimu kila kitu kinatakiwa kuonekana kwa rangi yake kama ni maji basi yaonekane na mtu aonekane.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.