Binti wa Angelina Jolie aichakaza mitandao ya kijamii

Mtoto wa mwigizaji Angelina Jolie na Brad Pitt anayejuliakana kwa jina la Shiloh Jolie, ameibua gumzo katika mitandao ya kijamii huku jina lake likishika vichwa vya habari mbalimbali baada ya kuingia rasmi katika tasnia ya burudani kama wazazi wake.
Shiloh mwenye umri wa miaka 19 ameonekana katika kionjo cha video ya wimbo mpya wa Dayoung msanii kutoka kundi la WJSN uitwao “What’s a Girl to Do.” Huku ya wimbo huo ikitarajiwa kuachiwa leo Aprili 7, 2026.
Kwa mujibu wa kampuni ya Starship Entertainment, Shiloh alichaguliwa kupitia usaili uliyofanyika Marekani wakati wakutafuta dansa atakayeweza kufiti katika video hiyo. Inaelezwa kuwa alifanikiwa kupenya hadi hatua ya mwisho na kuchaguliwa kushiriki bila wahusika kujua kuwa anatoka katika familia ya mastaa wakubwa wa Hollywood.
“Tulichagua wasanii kupitia usaili wa wazi, na Shiloh alifanikiwa hadi hatua ya mwisho. Hata baada ya kurekodi hatukujua kama ni mtoto wa Angelina Jolie na Brad Pitt hadi tulipogundua baadaye,” ilieleza taarifa hiyo.
Katika kipande hicho cha video, Shiloh anaonekana akiwa na muonekano wa kuvutia, akiwa amesuka nywele mbili muonekano uliosambaa kwa kasi mitandaoni na kuwafanya mashabiki wengi kumfananisha na mama yake, Angelina Jolie. Aidha, baadhi ya vipande vya video hiyo vinaonesha uwezo wake mkubwa wa kudansi, jambo ambalo liliwavutia Zaidi mashabiki.
Hii si mara ya kwanza kwa Shiloh kuonyesha kipaji chake hadharani. Mei 2024, mwalimu wake wa dansi Lil Kelaan Carter alishare video yake kupitia Instagram ikimuonesha akidansi wimbo wa ‘Tanzania’ wa Uncle Waffles aliomshirikisha Tony Duardo, Sino Msolo na Boibizza.
Mbali na hilo, Juni 2022 aliwahi kuonekana akicheza katika studio ya Millennium Dance Complex iliyopo jijini Los Angeles, video ambayo ilirekodiwa na mwalimu wa dansi Hamilton Evans ikimuonesha anacheza wimbo wa ‘Vegas’ wa Doja Cat.
Aidha mmoja wa wakufunzi wake wa dansi aitwaye Kolanie Marks ameliambia jarida la People kuwa Shiloh ni mwanafunzi ambaye aikuwa na juhudi na mwenye kujituma sana.

“Ni mtu ambaye nimefanya naye kazi kwa miaka kadhaa sasa. Mtindo wangu wa dansi ni mgumu kwa watu wengi, lakini yeye amejitoa kuhakikisha anaujua, ni mwanafunzi ambaye anajituma sana katika Sanaa naamini atafika mbali,” alisema Marks
Kuibuka kwa Shiloh katika soko la K-pop kunaonekana kuwa hatua kubwa katika safari yake ya sanaa, huku wengi wakiamini anaweza kujitengenezea jina lake binafsi mbali na umaarufu wa wazazi wake.
Shiloh Jolie ni mtoto wa pili wa Angelina Jolie na Brad Pitt kati ya watoto sita ambao wote wamewapata katika ndoa na uhusiano wao. Ndugu zake wengine ni pamoja na Maddox Jolie-Pitt, Pax Jolie-Pitt, Knox Jolie-Pitt, Vivienne Jolie-Pitt na Zahara Jolie-Pitt ambaye walimuasili.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.