Shati hili linauzwa Sh 2.8 milioni

Chapa ya mavazi kutoka Uswizi ‘Vetements’, imeibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuzindua shati jeupe la kawaida lenye mchoro unaofanana na alama ya kuungua kwa pasi, huku bei yake ikiwavuruga wengi.
Shati hilo lililopewa jina la ‘White Ironing Burn Graphic Shirt’ kwanza ni pana ‘ (oversized fit), lakini pia lina alama kwenye mfuko wa kifuano, alama au doa ambalo linatokana na kuunguzwa kwa pasi. Ubunifu huo wa kipekee umeibua hisia tofauti, huku baadhi wakipendezwa nao wengine wakiuponda.

Shati hilo linauzwa dola 1,139 za Marekani, ikiwa ni zaidi ya Sh 2.8 milioni. Jambo ambalo limezua mjadala mkubwa kuhusu thamani ya vazi hilo.
Baada ya picha za shati hilo kusambaa mtandaoni, watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walitoa maoni yao hasa wakiongelea gharama, wakiandiaka “Kwa nini nilipie zaidi ya dola 1,000 wakati ninaweza kuchoma shati langu mwenyewe?” huku mwingine akiandika, “Mama yangu alinifanyia hii bure kabisa.”
Aidha wengine wameiponda chapa wakiandika “Tatizo lake ni kukosa ubunifu na linaonekana chafu tu. Wabunifu wakubwa hutengeneza vitu vya kiwango cha juu, lakini hiki ni cha kawaida sana. Bei yake ilipaswa kuwa sifuri. Labda kama ingekuwa fulana ya utani ingeweza kueleweka, lakini si shati jeupe,”
Mwingine aliandika, “Hapa ndipo mitindo inaacha kuwa sanaa na inaanza kuwa mzaha. Hununui shati tu, unanunua uwezo wa kusema umetumia dola 1,139 kwa uharibifu wa bandia.”
Licha ya ukosoaji huo, Vetements imeendelea kujulikana kwa kuwasilisha mitindo isiyo ya kawaida inayochochea mjadala, jambo linaloonyesha jinsi tasnia ya mitindo ya kifahari inavyozidi kuvuka mipaka ya ubunifu wa kawaida.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.