-->

Breaking News

Patoranking amewataja Alikiba na Diamond kama wanajeshi

 Patoranking amewataja Alikiba na Diamond kama wanajeshi

Katika wimbo wake mpya wa African Soldier, msanii kutoka Nigeria, Patoranking amewataja nyota wawili wa Tanzania, Ali Kiba na Diamond Platnumz kama wanajeshi.

Hii ni heshima kubwa sana kwa Bongo Flava kuona wasanii wake wanatambuliwa kwa kiwango hicho.

Hata hivyo, kama Patoranking anawaona nyota hawa ni wanajeshi wa Afrika, basi Diamond Platnumz ni zaidi ya mwanajeshi, ni dege kubwa la jeshi aina ya Stealth aircraft.

Stealth Aircraft Nini?
Kwenye vita dhidi ya Iran, Marekani wametumia ndege hatari ya kivita ya kizazi cha tano inayoitwa F 22 Raptor. Ndege hii hatari zaidi duniani, ina uwezo wa hali ya juu wa kujificha na kupotea kwenye rada.

Uwezo huu ndio huitwa Stealth... Ni ndege chache sana zenye sifa hii. Kimsingi kuna ndege ya aina mbili tu zenye uwezo wa stealth; Stealth Fighters na Stealth Bombers.
(I). Stealth Fighter
Ndege hii sifa yake ni kasi, unyumbulifu na imebuniwa maalumu kushinda udhibiti wa angani kupambana na ndege za adui na shabaha za ardhini. F-22 na F-35 ni mfano ya ndege hii.

(Ii). Stealth Bomber
Ndege hii ni kubwa, ya masafa marefu na yenye kasi ya hali ya juu kiwango cha kati. Zimebuniwa maalumu kupenya ndani kabisa kwenye mipaka ya adui kutupa mabomu ya kawaida na hata ya nyuklia. Mfano wa ndege hii ni B-2 na B-21.
Sasa uwezo wa kujificha na kutoonekana hata kwenye rada yaani Stealth, ndio sifa za Diamond Platnumz. Haya sio maneno yangu bali ni yeye mwenyewe anavyojichukulia.

Angalia picha hii kisha linganisha na zile mbili za juu za ile midege. (Weka picha ya Diamond Platnumz). Huyu ni Diamond Platnumz na hii ni mwaka 2015 kwenye kampeni za CCM (picha kwa hisani ya Makinikia ya Issa Michuzi).

Yaani miaka zaidi ya 10 iliyopita Diamond Platnumz alijiona sawa na ndege za kivita... Unamuwezaje huyu mtu?
Kama ambavyo Marekani inazitegemea zile ndege zake kwenye vita vya angani, ndivyo Bongo Flava inavyomtegemea Diamond Platnumz kupasua anga la kimataifa.
Diamond Platnumz ana uwezo wa Stealth, kujificha na kutoonekana kwenye rada na kisha kuangusha bomu la maangamizi.



Unakumbuka KOMASAVA, lile lilikuwa bomu la hatari sana. Dunia nzima ilisalimia kwa lugha mbalimbali na ikafurahi. Ni anga gani la kimataifa Diamond Platnumz hajalichana? Ana sifa zote za zile ndege za aina zote mbili; yaani stealth fighter na stealth bomber.

Diamond Platnumz ni sawa na Stealth Fighter, ile ndege yenye sifa ya kasi, unyumbulifu na nguvu ya udhibiti wa angani kupambana na ndege za adui na shabaha za ardhini. Nyimbo zake ngapi zimepenya kimataifa na kushika chati ya juu duniani?

Pia Diamond Platnumz ni Stealth Bomber, ile ndege yenye sifa kufanya mashambulizi ya masafa marefu na yenye kasi ya hali ya juu zenye kupenya ndani kabisa kwenye mipaka ya adui kutupa mabomu hata ya nyuklia.

Ni nyimbo ngapi za Diamond Platnumz zimepenya ndani kabisa ya ngome za watu wa nje na kushika chati?
Hivi karibuni ilisambaa mitandaoni video ya wachezaji wa Chelsea, Cole Palmer na Marc Cucurella wakiwa kwenye klabu moja ya usiku huko Dubai, wimbo unaosikika ni wa Diamond Platnumz. Hii ndio maana ya stealth... ndege imepenya hadi Dubai na inasumbua.

Mwaka 2020, Diamond Platnumz alikuwa msanii wa kwanza kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kufikisha watazamaji bilioni moja kwenye YouTube. Na huko ndiko Diamond anasumbua vibaya zaidi, huku nyimbo zake kadhaa zikitamba.

"Yope" (Remix) (feat. Innoss'B): Hii ni moja ya nyimbo zake maarufu zaidi, ukivutia watazamaji zaidi ya milioni 250 kwenye YouTube. "Waah!" (feat. Koffi Olomide): Wimbo mkubwa uliovutia watazamaji zaidi ya milioni 170 YouTube.



"Inama" (feat. Fally Ipupa): Wimbo mwingine wa balaa uliovutia watazamaji zaidi ya milioni 150. "Komasava" (Comment Ça Va) (feat. Khalil Harrison, Chley Nkosi): Hii ilikuwa homa ya dunia na uliwasilishwa kuwania tuzo ya Grammy.

"African Beauty" (feat. Omarion): Wimbo mkubwa uliopenya nje ya Afrika, ukinyonywa zaidi ya mara milioni 20 kwenye mitandao mbalimbali ya biashara ya muziki.
"Marry You" (feat. Ne-Yo): Wimbo mwingine mkubwa uliopasua anga za kimataifa za R&B, kama bomu lililotupwa na zile ndege.

Hakuna msanii wa Afrika Mashariki mwenye kuweza kupenya angalau nusu ya Diamond Platnumz kwa sasa... na itachukua miaka mingi sana kumpata.

Kama ambavyo ndege tajwa hapo iligunduliwa baada ya vita vya dunia... hadi leo bado inatamba na Diamond Platnumz itakuwa hivyo... kazi zake zitatamba kwa miaka mingi ijayo bila kutolewa za kuzifunika.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.