Trending

Search Suggest

Chuck Norris afariki dunia akiwa na umri wa miaka 86

Chuck Norris afariki dunia akiwa na umri wa miaka 86

 


.

Chanzo cha picha,Getty Images

Mwigizaji na msanii wa mapigano ya judo, Chuck Norris alifariki dunia jana asubuhi akiwa na umri wa miaka 86, familia yake imetangaza kupitia mtandao wa Instagram.

Norris alilazwa hospitalini huko Hawaii kabla ya kifo chake

Norris alilazwa hospitalini huko Hawaii kwa dharura ya kimatibabu kabla ya kifo chake, TMZ iliripoti hapo awali.

Katika taarifa yao, familia yake ilisema wanapendelea kuweka hali hiyo kuwa ya siri, lakini walielezea kifo cha Norris kama kilichotokea "ghafla".

'Hamkuwa mashabiki tu, mlikuwa marafiki zake' - taarifa kamili ya familia

Tunasikitika kama familia kutangaza kifo cha ghafla cha mpendwa wetu Chuck Norris kilichotokea jana asubuhi. Ingawa tungependa kuweka hali hiyo kuwa ya faragha, tafadhali jua kwamba alikuwa amezungukwa na familia yake na alituacha akiwa na amani.

"Kwa ulimwengu, alikuwa msanii wa mapigano ya judo, mwigizaji, na nembo ya nguvu. Kwetu, alikuwa mume aliyejitolea, baba na babu mwenye upendo, ndugu wa kipekee, na kitovu cha familia"

Aliishi maisha yake kwa imani, kusudi, na kujitolea bila kuyumba kwa watu aliowapenda. Kupitia kazi yake, nidhamu, na wema wake, alitoa hamasa kwa mamilioni duniani kote na mchango wake utakumbukwa na wengi daima.

Ingawa mioyo yetu imeumia, tunashukuru sana kwa maisha aliyoishi na kwa nyakati zisizosahaulika tulizobarikiwa kushirikishana naye. Upendo na uungwaji mkono aliopata kutoka kwa mashabiki kote ulimwenguni ulikuwa na maana kubwa kwake, na familia yetu inawashukuru sana kwa hilo. Kwake, hamkuwa mashabiki tu, mlikuwa marafiki zake.

Tunajua wengi wenu mmesikia kuhusu kulazwa kwake hospitalini hivi karibuni, na tunashukuru sana kwa maombi na usaidizi mliompa.

Tunapoomboleza msiba huu, tunaomba faragha kwa ajili ya familia yetu wakati huu. Asante kwa kumpenda pamoja nasi.

Post a Comment