RASMI beki wa kazi ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Steve Barker ameanza mazoezi maalumu ili kurejea katika ubora.
Ni Abdulrazack Hamza ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Anatarajiwa kuwa nje kwa msimu mzima akipambania hali yake ikiwa atatengamaa mapema kuna uwezekano akarejea katikati ya msimu.
Licha ya kuanza mazoezi hayo ni wazi kwamba atakosekana kwenye mchezo ujao wa ligi ugenini ambapo timu ya Simba SC ipo Mwanza.
Machi 19,2026 ni Pamba Jiji FC vs Simba SC mchezo wa NBC Premier League ambapo beki huyo hayupo kwenye mpango wa benchi la ufundi kwa kuwa bado hawajawafiti.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.