Bayern Munich Wawasha Moto Ulaya, Je Kompany Ataibuka na Makombe Mangapi?

Huu ni msimu bora kabisa kwa timu ya Ujerumani, Bayern Munich ambao wamekuwa kwenye mwendelezo wa kufanya vizuri Ulaya na hata ligi ya ndani. Je Kompany na vijana wake watachukua Makombe mangapi msimu huu?
Klabu hii imeendelea kuonesha ubora wake msimu huu, ikionesha kuwa ni miongoni mwa nguvu za soka la Ujerumani na Ulaya.
Bayern chini ya Vicent Kompany imeendelea kufanya vyema katika Ligi ya Bundesliga, ikishika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi huku ikitaka kushinda mataji yote kwenye mashindano wanayoshiriki.
Chini ya kocha huyo kikosi hicho kimekuwa bora zaidi huku wakiwa na safu bora ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Harry Kane aliyefikisha magoli 50 kwenye mechi 42 alizocheza hadi sasa.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.