-->

Breaking News

Baada ya kumalizana na Diamond, sasa zamu ya Alikiba

 Baada ya kumalizana na Diamond, sasa zamu ya Alikiba


Nyota kutoka Rwanda, Bruce Melodie, ambaye aliwahi kutamba na wimbo aliomshirikisha Diamond Platnumz na kupata mafanikio makubwa, sasa amehamishia nguvu upande mwingine akiingia studio na nguli wa Bongo Fleva, Alikiba.

Kupitia ukurasa wa instagram wa msanii huyo ameshare picha akiwa studio na Alikiba ikiwa ni ishara ya uwezekano wa ujio wa kazi moya ya pamoja. Huku akiandia..



“Ni baraka kila mara kuungana na ndugu yangu King Kiba. Pamoja, tutaendelea kuinua muziki wa Afrika Mashariki kwenda viwango vya juu zaidi 🎶🌍 #Munyakazi”

Hatua hii imepokelewa kwa shauku kubwa na mashabiki, wengi wakisubiri kwa hamu kuona matokeo ya ushirikiano huo mpya kati ya wasanii hao wawili wakubwa kutoka Afrika Mashariki.

Wimbo ambao Bruce Melodie amemshirikisha Diamond Platnumz, pamoja na Brown Joel, video yake ilifanyika hapa hapa Bongo na kufanikiwa kutazamwa na watu zaidi ya milioni 7.2 ndani ya miezi miwili tu tangu kuachiwa kwake.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.