Hatimaye Dayna Nyange amempata!

“Watu walikuwa wakiniambia kuwa mimi ni mtu wa kuchagua sana, nami nikawaambia kuwa si wa kuchagua bali najua ninachokitaka. Leo niliwaambia kuwa nimekupata”.

“Wewe ndiye ninayemtaka, wewe ndiye niliyemuomba kwa Mungu — WEWE NDIWE AMINA YANGU!”
“Wewe ni jibu la maombi yangu, wewe ni kila nilichokitaka na zaidi. Nashukuru sana kuwa nawe, na nina furaha kubwa na hamasa ya kutumia maisha yangu yote nikiwa pamoja nawe.

“Nakuchagua leo, kesho na milele. Nakupenda leo, kesho na daima.” – Dayna Nyange kupitia Instagram.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.