BEKI aliyekuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC ya Dar tayari ameanza kazi ndani ya Singida Black Stars ikiwa ni majukumu mapya.
Anaitwa Abdalah Said maarufu kwa jina la Lanso beki aliyekuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha KMC kinachotumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani.
Lanso tayari ni mchezaji mpya ndani ya matajiri wa Alizeti kutoka Singida ambao hutumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani.
Beki huyo ameanza changamoto mpya katika dirisha dogo la usajili akiwa ndani ya Singida Black Stars iliyogotea hatua ya nusu fainali NMB Mapinduzi Cup 2026 ikiondolewa na Yanga SC.
Lanso alijiunga na KMC akitokea Mlandege ya Zanzibar, alicheza mchezo wa nusu fainali na alifanikiwa kutimiza majukumu yake eneo la ukabaji akipambana na kiungo Pacome aliyetoa pasi ya goli kwa Maxi Nzengeli kwenye mchezo huo.
Januari 12 2026, Singida Black Stars imemtambulisha nyota mwingine ambaye ni mshambuliaji anaitwa Steven Mboni ambaye tayari ameanza kazi.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.