CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
West Ham wanaweza kumnunua Nuno Espirito Santo iwapo watamtimua Graham Potter, Arsenal miongoni mwa timu zinazomtaka Luiz Gustavo Benedetti na Manchester United inaonyesha nia ya kumnunua Elliot Anderson.
West Ham wanafikiria kumnunua Nuno Espirito Santo iwapo watamtimua meneja Graham Potter. (Alan Nixon)
Arsenal, Barcelona na Napoli wanavutiwa na beki wa kati wa Palmeiras mwenye umri wa miaka 19 Mbrazil Luiz Gustavo Benedetti. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Manchester United wanavutiwa na kiungo wa kati wa Nottingham Forest Elliot Anderson mwenye thamani ya pauni milioni 70, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 22, ana furaha katika Uwanja wa City Ground na hana mpango wa kuondoka. (Football Insider)
Chelsea walikuwa na ofa ya pauni milioni 70 kwa ajili ya mshambuliaji wa Juventus Kenan Yildiz iliyokataliwa msimu wa joto, huku timu hiyo ya Italia ikitumai kumsaini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki mwenye umri wa miaka 20 chini ya mkataba wa muda mrefu. (Calciomercato – In Itali)
Crystal Palace wanaweza kufikiria ofa za pauni milioni 60 kwa Adam Wharton mwezi Januari, huku Liverpool wakimtaka kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 21. (TeamTalks)
Manchester United itachuana na Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa pembeni wa Inter Milan, 29, Denzel Dumfries. (Football Insider)
Real Madrid wanafuatilia maendeleo ya winga wa Leicester mwenye umri wa chini ya miaka 19 Jeremy Monga, 16. (Fichajes – In Spanish)