CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Ruben Amorim anakabiliwa na kipindi kigumu kama mkufunzi wa Manchester United, huku mechi tatu zijazo zikiamua iwapo atasalia kuinoa Old Trafford au la. (Daily Express)
Meneja wa Crystal Palace Oliver Glasner, mkufunzi wa zamani wa England Gareth Southgate, mkuu wa Fulham Marco Silva na Iraola wa Bournemouth ni miongoni mwa wanaoweza kuchukua nafasi ya Amorim iwapo Manchester United itamfukuza. (Daily Star)
West Ham pia wameanza kufikiria warithi wa kocha Graham Potter ambaye hana presha na wanataka mtu ambaye anaweza kukichangamsha kikosi na mashabiki wa klabu hiyo. (TeamTalks)

Newcastle wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United mwenye umri wa miaka 20 kutoka Uingereza Kobbie Mainoo Januari. (Talksport
Real Madrid na Paris St-Germain wanafuatilia hali ya William Saliba katika klabu ya Arsenal, huku mazungumzo yakiendelea kuhusu mkataba mpya wa beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. (CaughtOffside)
Chelsea wanaongeza jitihada zao za kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace Adam Wharton mwenye umri wa miaka 21 mwezi Januari. (Teamtalks)
Everton huenda wakaingia kwenye soko la uhamisho la bila malipo kwa beki wa pembeni ikiwa matatizo yao ya jeraha yataendelea. (Football Insider)
West Ham, Everton na Nottingham Forest walifikiria kumnunua Sergio Reguilon msimu wa joto, huku mlinzi huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka Tottenham. (Mail)

Liverpool wanafikiria mchezaji wa kimataifa wa Barcelona na Uruguay Ronald Araujo kuchukua nafasi ya mlinzi mwenzake Ibrahima Konate mwenye umri wa miaka 26 iwapo Mfaransa huyo ataondoka kwenda Real Madrid. (Fichajes - In Spanish)
Bournemouth inakusudia kuongeza mazungumzo ya kandarasi na kocha mkuu Andoni Iraola mwezi ujao huku mkataba wa sasa wa Mhispania huyo ukikamilika msimu ujao wa joto. (The I paper - Subscription Required)
Wakala wa mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson anasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hatarejea Chelsea kufuatia uhamisho wake wa mkopo kwenda Bayern Munich. (Canal+ via Transfermarkt - in German), external