CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland amekuwa kivutio kikuu kwa rais wa Barcelona Joan Laporta, ambaye ana uhakika mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway, 25, atajiunga na klabu hiyo ya La Liga siku zijazo. (El Nacional - In Spanish),
Manchester City wako tayari kushindana na Liverpool kwa ajili ya kumsajili bila malipo mlinzi wa England na Crystal Palace Marc Guehi mwenye umri wa miaka 25 msimu ujao, mkataba wake utakapokamilika. (Mirror)
Brentford wameonyesha nia ya kutaka kumnunua beki wa pembeni wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 19 Almugera Kabar. (Bild - In Deutch, Subscription Required)

Everton itakataa mbinu zozote za kumnunua beki wa kati wa England Jarrad Branthwaite 2026 huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akiwa sehemu ya mradi wa muda mrefu katika klabu hiyo. (Talksport)
Skauti kutoka Arsenal, Chelsea, Manchester United, Barcelona na Real Madrid wote wamekuwa wakimtazama kiungo wa kati wa Ajax na Ubelgiji Jorthy Mokio mwenye umri wa miaka 17. (Caughtoffside)
Kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 21, ana nia ya kutaka kujiunga na Liverpool licha ya kutakiwa na Real Madrid, Chelsea na Manchester United. (Fichajes - In Spanish)

Mgombea urais wa Benfica Cristovao Carvalho anasema kuwa atamfukuza kocha Bruno Lage na kujaribu kumshawishi kocha wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp kuchukua nafasi yake iwapo atachaguliwa mwezi ujao. (Sportbild - In Germany), nje
Mgombea mwingine wa urais wa Benfica Joao Noronha Lopes anataka kumrudisha kocha wa Manchester United Ruben Amorim katika klabu hiyo ya Lisbon, ambako alikaa miaka tisa kama mchezaji. (Times - Subscription Required)