A Zeno.FM Station Meja Kunta, Makabila Kusindikiza Shoo Ya Doumbia, Pacome

Meja Kunta, Makabila Kusindikiza Shoo Ya Doumbia, Pacome

IDDY AMAN
0

Wakali wa Singeli, Meja Kunta, Dulla Makabila na Mzee wa Bwax ni baadhi wasanii watakaosindikiza shoo ya utambulisho wa kikosi kipya cha Yanga chenye nyota kama Mohammed Doumbia na Pacome Zouzoua.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amewataja wasanii watakaotumbuiza katika kilele cha Wiki ya Mwananchi kinachofanyika kesho wakiongozwa na Zuchu.

Kamwe amesema ukiomuondoa Zuchu kesho pia kutakuwa na Meja Kunta, Dullah Makabila, Mzee wa Bwax na D Voice.

Akizungumza mapema leo, Kamwe amesema kwa upande wa Singeli wamebeba wasanii wote bora na watafanya kazi bora eneo la burudani.
"Kila mmoja anatambua ubora wa wasanii niliowataja hapo juu njooni mshuhudie kitu bora ndani ya Mkapa wasanii wamejiandaa kukata kiu ya burudani."

Akimzungumzia Zuchu amesema mwanadada huyo ataenda kuonyesha utofauti wa wasanii wanaotakiea kutoa burudani uwanjani na katika harusi.

"Nimeshuhudia maandalizi yote aliyoyafanya Zuchu mashabiki watarajie kitu kikubwa na bora na ndio daraja la ubora litajengwa hapo," amesema Kamwe na kuongeza;

"Zuchu amepania hili tamasha maandalizi aliyoyafanya nikisema nielezee hapa ntaharibu ubora mkubwa utakaotarajiwa kuonyeshwa,”
 

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default