-->

Breaking News

Yanga wampiga chini Yao Kuoussi huyu hapa mrithi wake

 


Rasmi klabu ya Yanga leo imetambulisha usajili wa beki wa kati Frank Assinki aliyetua kutoka klabu ya Singida Black Stars

Assinki alitua Dar jana na moja kwa moja kuelekea Avic Town baada ya kumalizana na mabosi wa Yanga

Beki huyo raia wa Ghana anachukua nafasi ya Yao Kouassi ambaye anaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti

Assinki anakwenda kuimarisha safu ya ulinzi ya Yanga akiungana na mabeki wengine wa kati Dickson Job, Ibrahim Hamad na Bakari Mwamnyeto. Yanga haina masihara na safu yake ya ulinzi...!

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.