Simba yasongeza mbele Tarehe ya uzinduzi wa jezi
Klabu ya Simba Sc imetangaza kusogeza mbele tukio la uzinduzi wa jezi za klabu hiyo kutoka Agosti 27, 2025 kama ilivyopangwa awali na sasa hafla hiyo ya uzinduzi itafanyika Agosti 31, 2025, sababu ya mabadiliko hayo haijatajwa.
Awali Wekundu hao wa Msimbazi walitangaza kuwa uzinduzi wa jezi hizo kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/26 itafanyika Agosti 27, 2025 katika ukumbi wa SuperDome, Masaki kuanzia saa 1 usiku huku ikitaja kiingilio cha Tsh. 250,000 kwa shabiki anayetaka kuhudhuria uzinduzi huo.
#Baada ya tambara kuvuja wameamua kwenda kufanya marekebisho hawa makolo

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.