-->

Breaking News

Simba kurejea Tanzania leo, Yafunga mahesabu hivi

 


 Kikosi cha Simba kimehitimisha pre-season nchini Misri ambapo leo timu inatarajiwa kurejea nchini kuhitimisha awamu ya mwisho ya maandalizi

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amepata takribani wiki nne kukiandaa kikosi chake kambi ikianzia mji wa Ismailia na kisha kuhitimishwa Cairo

Sehemu kubwa ya wachezaji wamepata wa kutosha wa maandalizi ukiondoa wachezaji wachache ambao walichelewa kutokana na changamoto za vibali huku kiungo Neo Maema akitua baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu ya Taifa ya Afrika Kusini kwenye michuano ya CHAN 2024

Baada ya kurejea nchini Simba itakuwa na wiki moja zaidi ya kujiandaa kabla ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika Septemba 10

Mnyama atakuwa siku nyingine chache za kujiandaa kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambao mpaka sasa ratiba inaonyesha utapigwa Septemba 16

Baadae Simba itaelekea Botswana kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United utakaopigwa Septemba 20

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.