-->

Breaking News

Simba kuhitimisha pre-Season kwa mechi mbili za kibabe

 


 Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini Alhamisi, August 28 baada ya kukamilisha maandalizi ya mwezi mmoja ya pre-season huko Misri.

Simba itahitimisha kambi hiyo kwa kucheza mechi mbili za kirafiki, leo na kesho.

Leo Simba itamenyana na Wadi Degla katika mchezo utakaopigwa jijini Cairo, kabla ya kukamilisha maandalizi kwa mchezo wa kesho dhidi ya FS Fassel.

Wadi Degla inashiriki Ligi Kuu ya Misri huku Fassel wakiwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Algeria.

Mechi hizo zitampa nafasi Kocha Fadlu Davids kufanya tathmini ya mwisho ya kikosi chake kabla ya kurejea nyumbani.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.