Kocha Fadlu Afafanua Mustakabali wa Ladack Chasambi
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, ametoa msimamo wake wazi juu ya kiungo mshambuliaji, Ladack Chasambi, akibainisha kuwa hayupo katika mipango yake ya msimu ujao.
Inaelezwa kuwa Fadlu hana mpango wa Chasambi katika nafasi ya winga, na hivyo amempa chaguo muhimu: kama Chasambi anataka kubaki klabuni, basi lazima ajitahidi kubadilika na kuonyesha uwezo katika nafasi ya beki wa kulia.
Chanzo chetu kilieleza kuwa, kocha Davids pia amefungua mlango wa kuondoka kwa kiungo huyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho, ikiwa akipata ofa nzuri kwingine.
.webp)
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.