-->

Breaking News

Chungu na tamu ya soka la Bongo


 Ukisikia mwamba huyu ana roho ya kitajiri. Siyo ofa za pombe na wanawake. Bali kutoa pesa kwa lengo la kuingiza pesa zaidi. Tajiri wa kweli huwekeza kwenye muda. Muda na pesa ni kulwa na doto au mwili na maji.


Roho za kitajiri tofauti na roho za Malofa. Na hii ndo hufanya dunia iwe na matajiri wachache kuliko masikini. Masikini hutumia muda wao kumaliza pesa, (kujiliwaza). Mtajiri hutumia pesa kumaliza muda wao.


Sasa wenye mioyo ya kitajiri tajiri. Hawaoni hatari kuweka mzigo wa pesa sehemu. Mwa matumaini ya kupata mzigo mkubwa mbeleni. Utajiri ni kipawa. Huwezi kuwa tu tajiri  na mawazo yako ya ngono zembe.

 
Uwekezaji mkubwa wa  Azam FC. Kwa roho za kilofa ni matumizi mabaya ya pesa. Lakini Azam 'suuni' utakuwa mradi mkubwa. Wanachofanya ni kujenga msingi. Kusaka 'ingejimenti' ya watu kwa maana ya mashabiki.

 Mashabiki wa Azam hutowaona leo. Kesho mashabiki watakuwa wengi. Na Azam hii haiwezi kuwa tishio chini ya Yusuf. Azam tishio ni ile ya mtoto wa Yusuf. Na hili siyo jambo la leo wala kesho. Ila inaweza kuwa muda mfupi ujao...

 Kwa sababu Yusuf ni mmiliki siyo shabiki wa Azam. Ila mtoto wake atakuwa mmiliki na shabiki wa Azam. Na hapo balaa litaanza kuwa kubwa. Hata mimi nikiwa na timu, nitakuwa mmiliki tu, ushabiki utabaki Kariakoo.

 Mtoto wa Yusuf hawezi kuwa shabiki wa Simba au Yanga. Kwa kawaida anaipenda timu ya baba yake. Ndiyo, huu ndo ukweli ulio wazi. Kwa sasa Azam ni mradi tu. Matunda yake yapo wakati bosi akiwa shabiki wa Azam siyo mmiliki tu. 

 Hata Roma haikujengwa siku moja, ni hatua kwa hatua. Azam itakuwa balaa kwa bosi mwenye mahaba nayo. Bapo ndipo mradi wa Azam Fc utatawala soka la Bongo. Kwa sasa ni kama pambo ndani ya nyumba ya mtu.

 Simba na Yanga hudumaza sana makuzi ya timu zingine. Kama siyo ushabiki wa mabosi kwa vilabu vya Kariakoo. Leo Azam ingekuwa kama Pyramids. Shida nyingi chanzo ni uwepo wa Simba na Yanga. Mila sehemu vimelea vya Simba na Yanga vipo.

 

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.