A Zeno.FM Station Uzito Wamponza Aziz K Wydad, Meneja Wake Afunguka

Uzito Wamponza Aziz K Wydad, Meneja Wake Afunguka


Uzito Wamponza Aziz K Wydad, Meneja Wake Afunguka

Aliyekuwa nyota wa Klabu ya Yanga SC, Stephane Aziz Ki, ambaye kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco, anaripotiwa kuwa katika wakati mgumu ndani ya kikosi hicho kutokana na kuongezeka kwa uzito, kupungua kwa kasi yake ya kawaida na pia kupoteza mipira mingi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Morocco, hali hiyo imeanza kuzua wasiwasi kwa benchi la ufundi la Wydad, kiasi cha kuibua uwezekano wa kiungo huyo kutemwa.

Aziz Ki alijiunga na Wydad kwa uhamisho wa bure kutoka Yanga SC, kufuatia makubaliano maalum yaliyokuwepo kati ya klabu hiyo ya Tanzania na meneja wa mchezaji huyo. Hii ina maana kuwa Yanga haikupokea kiasi chochote cha fedha kutokana na uhamisho huo.

Kwa sasa, mashabiki na wachambuzi wa soka wanatazama kwa jicho la karibu mwenendo wa nyota huyo ambaye alikuwa tegemeo kubwa kwa Yanga SC akiwa nchini Tanzania, lakini mambo yanaonekana kwenda kombo pindi alipovuka mipaka ya Afrika Mashariki.

WASIKIE YANGA
“Mkataba ambao Aziz KI aliusaini na Wydad wakati tunawapa ni wenye vipengele viwili miezi mitatu ya kwanza wanamuangalia ðŸ˜… wakijiridhisha na kiwango watatulipa kwa miaka miwili,”

MSIKIE MENEJA WA AZIZ KI
“Stephane Aziz KI huenda asiwe sehemu ya kikosi hicho msimu ujao kuna ishu anaisikilizia. Ikiwa Wydad watakamilisha usajili wa Lorch kama navyoambiwa anacheza kwa mkopo kutoka Sundowns, basi nafasi ya Aziz KI itazidi kuwa finyu, hali inayoweza kumfanya aondoke labuni hapo mapema kuliko ilivyotarajiwa, lakini bado tuna Ofa za klabu za Afrika Kusini.”


Tags :-

Post a Comment

0 Comments