Tetesi za Soka Ulaya: Rodrygo kumrithi Luis Diaz Liverpool? - IDDYNATION SITE

Breaking News

Tetesi za Soka Ulaya: Rodrygo kumrithi Luis Diaz Liverpool?

 RodrygoWinga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, ni mmoja wa nyota wa kumrithi Luis Diaz huko Liverpool iwapo winga huyo wa Colombia mwenye umri wa miaka 28 ataondoka Anfield (Florian Plettenberg).

Mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, anataka pauni 300,000 kwa wiki kusaini mkataba mpya Newcastle (Talksport).

Granit Xhaka amekubaliana masharti na Sunderland, huku klabu hiyo sasa ikiwa kwenye mazungumzo na Bayer Leverkusen kuhusu ada ya kiungo huyo wa Uswisi mwenye umri wa miaka 32 (Times).

Atalanta na Lazio wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester United na DenAtletico Madrid wameanza mazungumzo na Chelsea kuhusu mpango wa kumsajili Renato Veiga, huku Blues wakidai takriban pauni milioni 35 kumuachia beki huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 21 (Fabrizio Romanomark Rasmus Hojlund, 22 (Footmercato).

Everton wanavutiwa na beki wa kushoto wa Bayern Munich na Morocco Adam Aznou, 19 (Athletic).

Brentford wamekataa ofa ya kwanza ya pauni milioni 30 kutoka Newcastle kwa ajili ya mshambuliaji wa DR Congo Yoane Wissa, 28 (Tbrfootball).

Wolves wako karibu kukamilisha usajili wa winga wa Colombia Jhon Arias, 25, kutoka Fluminense na beki wa kulia wa Hispania Marc Pubill, 22, kutoka Almeria (Telegraph).

Manchester United wanamfuatilia beki wa kushoto wa Mali, Dan Sinate wa Angers, lakini hawana uwezekano wa kufanya uhamisho kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 hadi Januari mapema zaidi (Sun).

Everton wanavutiwa na Samuel Lino wa Atletico Madrid, huku klabu hiyo ya Hispania ikiwa tayari kupokea ofa kwa winga huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 (AS).


No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.