A Zeno.FM Station Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Jadon Sancho kuondoka Man United

Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Jadon Sancho kuondoka Man United

 .hatua ya winga wa manchester United na Uingereza Jadon Sancho kutaka kujiunga na klabu ya Juventus kunakaribia kukamilika huku vilabu hivyo viwili vikiwa vimekamilisha baadhi ya maelezo kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Tuttosport - In Italy)Juventus wako tayari kukubaliana na Manchester United kwa dau la euro 25m (£21.6m) kumnunua Sancho, ambaye yuko katika makubaliano kamili na wababe hao wa Serie A kuhusu kandarasi ya miaka minne yenye thamani ya euro 6m (£5.2m) kwa mwaka. (Sportmediaset - In Italy)

Liverpool wanapewa nafasi kubwa ya kumnunua kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 21, juu ya Tottenham - lakini sio hadi msimu ujao wa joto, kwani mchezaji huyo anataka kukaa mwaka mwingine Selhurst Park. (Sun Sunday)

Barcelona italipa mshahara wote wa mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford wa pauni 325,000 kwa wiki katika mkataba ambao unatarajiwa kumpeleka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 kwa klabu hiyo ya Uhispania kwa mkopo wa awali wa msimu mzima. (Times – Subscription Required ),

Manchester United na Newcastle wamemtambua mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, kama mchezaji wanayempa kipaumbele kufuatia msimu uliopita uliofanikiwa kwa mkopo Juventus. (Footmercato – In French), nje

Kipa wa Everton na England Jordan Pickford, 31, anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka minne katika klabu hiyo ya Merseyside. (Sun Sunday )

AC Milan wanatazamia kufunga mkataba na Brighton ili kumsaini beki wa kushoto wa klabu hiyo ya Equador Pervis Estupinan, 27, kama mbadala wa mlinzi wa Ufaransa Theo Hernandez, 27, baada ya kuhamia Al-Hilal. (Gianluca di Marzio),

Bayern Munich wanapiga hatua katika majaribio yao ya kumsajili fowadi wa Liverpool Luis Diaz baada ya ofa mbili kukataliwa, huku klabu hizo mbili zikitarajiwa kufanya mkutano hivi karibuni kuhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 28. (Bild - In Germany,}

Evan Ferguson yuko tayari kujiunga na Roma kwa mkopo kutoka Brighton baada ya timu hiyo ya Serie A kufikia makubaliano ya mdomo, ikiwa ni pamoja na chaguo la euro 40m (£34.6m) kumnunua mshambuliaji huyo wa Jamhuri ya Ireland mwenye umri wa miaka 20. (Fabrizio Romano)

Fenerbahce wamekubali mikataba ya kumnunua mlinzi wa Slovakia Milan Skriniar, 30, na kiungo mshambuliaji wa Uhispania Marco Asensio, 29, kutoka Paris St-Germain. (Footmercato - In French)

Mshambulizi wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 36, amekataa ofa kutoka kwa Al-Ettifaq baada ya kuondoka Al-Qadsiah na sasa anataka kujiunga na Marseille. (Footmercato - kwa Kifaransa), nje

Liverpool wamewasilisha ofa ya £69m pamoja na nyongeza - £78m kwa jumla - kwa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 23 Mfaransa Hugo Ekitike. (Sky Sports) ya picha,
Tags :-

Post a Comment

0 Comments