A Zeno.FM Station Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Tatu zamgombania Jack Grealish

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Tatu zamgombania Jack Grealish

 


s

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Jack Grealish

Tottenham, Newcastle na Napoli zote zinamfuatilia kiungo wa England Jack Grealish baada ya Manchester City kuweka bei ya pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 (Sun).

Newcastle United wanaendelea kuwa na matumaini ya kushinda mbio za kumsajili Marc Guehi, 24, huku klabu hiyo ikitaka kuimarisha kikosi chao kwa kumuongeza beki wa kati huyo wa England na Crystal Palace (GiveMeSport).

Crystal Palace wenyewe wako kwenye mazungumzo na Sporting kuhusu uwezekano wa mpango wao wa pauni milioni 45 kumnasa beki wa Ivory Coast Ousmane Diomande, 21 (Guardian).

Newcastle pia wamefanya mazungumzo mapya na Dominic Calvert-Lewin, 28, huku meneja Eddie Howe akiwa shabiki wa muda mrefu wa mshambuliaji huyo wa England aliyeondoka Everton baada ya mkataba wake kumalizika mwezi uliopita. Anasakwa pia na maslahi kutoka Manchester United (Talksport).

Beki wa West Ham mwenye umri wa miaka 29 kutoka Morocco, Nayef Aguerd, anasakwa kwa udi na uvumba na klabu ya Ufaransa Marseille msimu huu wa joto (L'Equipe).

Manchester United wamefanya jaribio la kumsajili kiungo wa Atalanta na Brazil Ederson, huku vilabu viwili vya Serie A Inter Milan na Juventus pia vikimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mwenye thamani ya takriban pauni milioni 44 (Goal).

Mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, hafikirii kuondoka Manchester United isipokuwa kama klabu itaamua kumuuza, huku Inter Milan ikiwa moja ya vilabu vilivyoonyesha nia ya kumsajili (Fabrizio Romano).

Wakati huo huo, Manchester United waliweka ada ya uhamisho ya pauni milioni 30 kwa Andre Onana kwa AS Monaco mwishoni mwa mwezi uliopita, lakini kipa huyo wa Cameroon mwenye umri wa miaka 29 anaonekana kwa asilimia kubwa atabaki klabuni (Mail).

Manchester United pia wanavutiwa na kiungo wa Nigeria Wilfred Ndidi, 28, ambaye anaripotiwa kuwa katika mkataba wake kuna kipengele cha kuuzwa kwa pauni milioni 9 kutokana na kushuka daraja kwa Leicester City, huku Fulham, Everton na Crystal Palace pia wakimwania (Tuttosport).

Beki wa Italia Davide Calabria, 28, pia anasakwa na Crystal Palace. Alikuwa kwenye kiwango bora akiwa kwa mkopo Bologna msimu uliopita lakini sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka AC Milan mkataba wake ulipoisha (Sky Sports).

Sunderland, Leeds United na Wolves wanavutiwa na kiungo wa Lens na timu ya Morocco Under-23 Neil El Aynaoui, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka AS Roma, Juventus na AC Milan kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 (Footmercato).

Meneja wa Slavia Prague Jindrich Trpisovsky amethibitisha kuwa El Hadji Malick Diouf yuko tayari kuondoka klabuni huku West Ham na Leeds zikihusishwa na beki huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 20 (Standard).




Tags :-

Post a Comment

0 Comments