Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Man Utd kumnasa Emi Martinez?
Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumsajili Emi Martinez lakini huenda wakakatishwa tamaa na dau la £40 milioni linalotakiwa na Aston Villa kwa kipa huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 32. (Mail)
Winga wa Colombia, Luis Diaz, mwenye umri wa miaka 28, bado ana dhamira ya kuondoka Liverpool katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi, na anatumai Bayern Munich watawasilisha tena ofa mpya katika siku chache zijazo ili kujaribu kuishawishi klabu hiyo ya England. (ESPN)
Newcastle wako hatarini kupitwa na Manchester City katika harakati zao za kumsajili James Trafford, kipa wa Burnley na timu ya taifa ya England mwenye umri wa miaka 22. (Telegraph)
Trafford ana hamu kubwa ya kurejea Manchester City majira haya ya kiangazi baada ya City kuingilia kati mpango wa Newcastle wanaotaka kumsajili kipa huyo (Football Insider
Newcastle wanapanga kumpa Tino Livramento mkataba mpya ili kuzuia nia ya Manchester City, ambao wako tayari kulipa £65 milioni kwa beki huyo wa kulia wa England mwenye umri wa miaka 22. (Times)
Tottenham kupambana na Liverpool katika harakati za kumsajili beki wa kati wa England kutoka Crystal Palace, Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph)
Matumaini ya Manchester United ya kumsajili Nicolas Jackson yameimarika baada ya mshambuliaji huyo wa Chelsea na Senegal, mwenye umri wa miaka 24, kukataa ofa kutoka AC Milan na Napoli kwa sababu anataka kubaki Ligi Kuu ya England. (Sun)
AC Milan wako karibu kufikia makubaliano na Brighton kuhusu usajili wa beki wa pembeni wa Ecuador mwenye umri wa miaka 27, Pervis Estupinan. (Athletic)
Juventus wataongeza juhudi zao za kumsajili winga wa England kutoka Manchester United, Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 25, baada ya winga wa Ubelgiji Samuel Mbangula, 21, na mshambuliaji wa Marekani Timothy Weah, 25, kuondoka klabuni hapo (Tuttosport)
Manchester United wanajiandaa kushindana na Manchester City kuwania saini ya kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Denmark, Morten Hjulmand, mwenye umri wa miaka 26. (A Bola)
Chelsea wanaonyesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa RB Leipzig, Xavi Simons, mwenye umri wa miaka 22, lakini huenda wakalazimika kuuza baadhi ya wachezaji kwanza ili kumpa nafasi raia huyo wa Uholanzi kwenye kikosi chao. (Telegraph)
West Ham wana nia ya kumsajili kipa wa Leicester City, Mads Hermansen, raia wa Denmark mwenye umri wa miaka 25, na wanatarajiwa kuwasilisha ofa rasmi hivi karibuni. (Sky Sports)
Sunderland na Fenerbahce bado wanaonyesha nia ya kumsajili Granit Xhaka licha ya Bayer Leverkusen kukataa ofa kutoka kwa vilabu vyote viwili kwa kiungo huyo wa Uswizi mwenye umri wa miaka 32. (Florian Plettenberg)
Napoli, AC Milan, Roma, Juventus na Inter Milan zote zinaonyesha nia ya kumsajili winga wa Liverpool na timu ya taifa ya Italia, Federico Chiesa, mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato)
Everton wamezungumza na Real Sociedad kuhusu uwezekano wa kumsajili winga wa Japan mwenye umri wa miaka 24, Takefusa Kubo. (Teamtalk)
Fulham wanatarajiwa kukamilisha usajili wa kipa wa Montpellier, Benjamin Lecomte, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 34, ndani ya siku chache zijazo. (L'Equipe )
Nottingham Forest wanaendelea kufanya kazi kukamilisha dili la kumsajili winga wa Uswizi kutoka Bologna, Dan Ndoye, mwenye umri wa miaka 22. (Guardian)
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.