
Bayern Munich wamewasilisha ofa ya euro milioni 52 (pauni milioni 44.7) kwa ajiliu ya winga wa Liverpool na Colombia Luis Diaz, 28 (Bild
Nottingham Forest wamekataliwa tena ofa yao kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford Yoane Wissa, 28, ikiaminika kuwa ni chini ya pauni milioni 25 walizowahi kutoa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Kongo mnamo Januari, Bees wanataka pauni milioni 50 (The Athletic).
Liverpool wako tayari kuanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, 23, ingawa klabu hiyo inahitaji kuidhinisha uhamisho wa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 26, ili kuwezesha dili hilo (Givemesport).
The Reds wamevutiwa na Ekitike lakini bei yake na hali ya mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, huko Newcastle pia inaweza kuwa sababu katika dili lolote (Tbrfootball).
Haraka ya Arsenal ya kumsajili mshambuliaji wa Sweden Viktor Gyokeres, 27, iko hatarini kuvunjika kwa sababu klabu hiyo haijawasiliana na Sporting kwa siku tatu (Abola).
Real Madrid wako tayari kumruhusu winga wa Brazil Rodrygo kuondoka msimu huu wa joto, lakini klabu hiyo itaacha uamuzi wa mwisho kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye anataka kubaki Ulaya (Fabrizio Romano).
Kufuatia kushindwa kwa Real kwenye Kombe la dunia la vilabu, kocha Xabi Alonso anataka kumuuza Rodrygo, pamoja na kiungo wa Hispania Dani Ceballos, 28, na kiungo wa Morocco Brahim Diaz, 25 (Fichajes).
Miamba hiyo ya Hispania inapanga kufanya dili la kumsajili beki wa Tottenham Hotspur Cristian Romero, 27, ambaye pia anasakwa na klabu pinzani ya Atletico Madrid (Fichajes).
Arsenal wanaaminika kuwa na uhakika kwamba kiungo mshambuliaji wa England Under-21 Ethan Nwaneri atasaini mkataba mpya licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kutakiwa na Chelsea na vilabu vya Ujerumani (Guardian).
Mazungumzo ya Napoli na Galatasaray kuhusuVictor Osimhen, 26, juu ya ada yake ya uhamisho yamekwama. Mshambuliaji huyo wa Nigeria alitumia msimu uliopita kwa mkopo na klabu hiyo ya Uturuki (Gianlucadimarzio).
Sunderland wako kwenye mazungumzo na winga wa Kiingereza Romaine Mundle kuhusu kusaini mkataba mpya, kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anasakwa na PSV Eindhoven (Sky Sports).
Bosi wa Fenerbahce Jose Mourinho anamtaka mshambuliaji wa Ubelgiji Leandro Trossard, huku Arsenal wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 (Fotospor).
Real Betis wanaendelea kuwa na uhakika wa kumsajili winga wa Brazil Antony kutoka Manchester United, ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kupunguza mshahara wake kwa kiasi kikubwa ili kuhamia klabu hiyo ya Hispania (Sport).
Mshambuliaji wa Kiingereza Jamie Vardy, 38, anatakiwa na aliyekuwa bosi wa West Brom Carlos Corberan, ambaye sasa ni kocha mkuu wa Valencia katika ligi ya La Liga (Givemesport)