A Zeno.FM Station Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Napoli yamtaka Garnacho

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Napoli yamtaka Garnacho

 


Alejandro Garnacho

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Alejandro Garnacho

Napoli wamerejea tena kumuwania winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 21, na wanatumai wanaweza kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa pauni milioni 45 (Mirror)

United wanaendelea kuwa na matumaini ya kukubaliana na Brentford na mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, kwa wakati ili mshambuliaji huyo awe sehemu ya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani (Sky Sports).

Mazungumzo ya Arsenal ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting na Sweden Viktor Gyokeres, 27, yanasuasuakutokana na tofauti ya maoni kuhusu thamani na masharti ya jumla (Independent).

Newcastle United wamekataa ofa ya tatu kutoka Leeds United kwa kiungo wa Kiingereza Sean Longstaff, 27 (Northern Echo).

Al-Hilal wanamtaka mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 22, ambaye pia anasakwa na Arsenal. Klabu hiyo ya Saudi Pro League pia inavutiwa na mshambuliaji wa Ufaransa wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, 28 (Sun).

Aston Villa na Brighton wanamfuatilia kiungo mshambuliaji mwenye kipaji kikubwa kutoka Benin, Rodolfo Aloko, 18, anayetoka klabu ya Kroatia NK Kustosija (Mail).

Manchester United wanatarajia kumuuza winga wa Kiingereza Jadon Sancho, 25, kwa ada ya uhamisho iliyopunguzwa kwa kiasi kikubwa (Givemesport).

Nottingham Forest na Crystal Palace ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu vinavyomfuatilia kiungo wa Manchester City na England wa timu ya taifa ya vijana ya U-21s, James McAtee, 22, msimu huu wa joto (Sky Sports).

Liverpool wanaweza kujiunga na Arsenal katika mbio za kumsajili winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, ikiwa wataishia kumpoteza winga wa Colombia Luis Diaz, 28, kwa Barcelona (Sacha Tavolieri via Goal).

Winga wa Ureno Chiquinho, 25, ameondoka Wolves kujiunga na Alverca nchini Ureno kwa mkataba wa kudumu, huku klabu hiyo ya Ligi Kuu ikibaki na kipengele cha asilimia 40 cha mauzo ya baadaye (Fabrizio Romano).

Brighton wako tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson kwenda Roma lakini klabu hiyo bado haijapata idhini kutoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 (Calciomercato).


Tags :-

Post a Comment

0 Comments