A Zeno.FM Station Fei Toto Aikana Yanga Mchana Kweupe, Adai Azam Bado Mabosi zake

Fei Toto Aikana Yanga Mchana Kweupe, Adai Azam Bado Mabosi zake


Fei Toto Aikana Yanga Mchana Kweupe, Adai Azam Bado Mabosi zake

TETESI za usajili zinadai kuwa Feisal Salum ‘Fei Toto’ amemalizana na Yanga SC, lakini kiungo huyo wa Azam FC ameibuka na kufunguka wazi kuhusu hatma yake kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Fei Toto amesema kwa sasa bado ni mchezaji halali wa Azam FC, akiwa na mkataba wa mwaka mmoja zaidi, hana mamlaka ya kuzungumzia mipango ya klabu nyingine yoyote.

“Siwezi kuzungumzia suala la Yanga, wala sifahamu kama kweli wameleta ofa au la, kwa sababu bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC. Mimi ni mchezaji wao hadi hapo nitakapomaliza mkataba wangu,” amesema kiungo huyo.

Kauli hiyo ya Fei Toto imekuja kufuatia taarifa zilizozagaa kwamba tayari amefikia makubaliano ya kurejea Yanga SC, klabu aliyoitumikia kabla ya kujiunga na Azam FC.

Inadaiwa kuwa viongozi wa Yanga wamekuwa kwenye mazungumzo na wenzao wa Azam FC kwa lengo la kumrejesha kiungo huyo katika kikosi chao, wakiamini anaweza kuimarisha safu ya kiungo msimu ujao.

Fei Toto alijiunga na Azam FC akitokea Yanga SC msimu wa 2023/24, kwa mkataba wa miaka mitatu. Uhamisho wake ulihusisha matarajio makubwa ya kuongeza ubora katika eneo la kiungo wa ulinzi ndani ya kikosi cha Azam.

Kwa sasa, mashabiki wa soka wanasubiri kwa hamu kuona iwapo tetesi hizo zitageuka kuwa kweli au la, huku suala la uhamisho wake likibaki mikononi mwa klabu husika na uongozi wake binafsi.

Tags :-

Post a Comment

0 Comments