Liverpool tayari imetumia zaidi ya pauni milioni 170 msimu huu wa kiangazi - na sasa wanamtaka mchezaji ambaye atawagharimu hela nyingi sana kumsajili.
Alexander Isak wa Newcastle United anakadiriwa kugharimu hadi pauni milioni 130, wakiamua kumsajili basi matumizi yao yatapanda kwa kiwango cha takriban £300m.
Hicho ni kiwango kikubwa sana.
Mabingwa hao wa Ligi ya Premia mwaka jana walitumia £10m kumsajili winga wa Italia Federico Chiesa na £25m kumsajili kipa wa Georgia Giorgi Mamardashvili wakati wa uhamisho wa wachezaji wa msimu wa kiangazi mwaka uliopita.
Liverpool tayari imemsajili kiungo Florian Wirtz kwa kima cha pauni milioni 116 katika kile kinachoonekana kuwa mkataba uliovunja rekodi msimu huu na kulipa pauni milioni 40 na pauni milioni 30 mtawalia kuwasajili mabeki Milos Kerkez na Jeremie Frimpong.