
Arsenal inaweza kujiondoa kwenye dili la pauni milioni 70 kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, mwenye umri wa miaka 22, kutokana na madai makubwa ya mshahara ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia. Mshambuliaji wa Sporting na Sweden, Viktor Gyokeres, mwenye umri wa miaka 27, anatajwa kuwa chaguo mbadala. (Mirror)
Bayern Munich wameingia katika mbio za kumnunua Jamie Gittens, mwenye umri wa miaka 20, ambaye anasakwa na Chelsea. Mabingwa hao wa Ujerumani wanaripotiwa kuwa tayari kutoa pauni milioni 55 kwenda Borussia Dortmund kwa ajili ya winga huyo. (Kicker)
Uhamisho kutoka Juventus kwa winga wa Manchester United, Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 25, unategemea kama klabu hiyo ya Italia itamsajili Francisco Conceicao kutoka Porto. (Corriere dello Sport)

Kwa upande wa Chelsea, Nicolas Jackson, mwenye umri wa miaka 24, hauzwi licha ya kuwepo kwa klabu zinazomtaka kutoka Saudi Arabia na Ulaya. (Sky Sports)
Liverpool wamekubali dili la kumuuza beki Jarell Quansah, mwenye umri wa miaka 22, kwenda Bayer Leverkusen kwa pauni milioni 35. Klabu hiyo imeweka kipengele cha kumnunua tena katika mkataba huo. (Fabrizio Romano)
End of Iliyosomwa zaidi
Manchester United wanaonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina na Italia, Moise Kean, mwenye umri wa miaka 25, ambaye ana kipengele cha kuuuzwa kwa euro milioni 52 (pauni milioni 44.5) katika mkataba wake, ambacho kitatumika kuanzia Julai 1 hadi 15. (La Gazzetta dello Sport)
Wrexham na Stockport County wanavutiwa na mshambuliaji wa zamani wa Wales na Rangers, Tom Lawrence, mwenye umri wa miaka 31. (Sky Sports)
Beki wa Denmark, Andreas Christensen, mwenye umri wa miaka 29, anatarajiwa kuondoka Barcelona msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)