Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Emiliano Martinez

Chelsea wamepewa fursa ya kumsajili kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez kwa pauni milioni 45, ingawa kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Argentina anaaminika kuwa anapendelea kuhamia Manchester United. (Mirror)

Manchester United wako tayari kuanza mazungumzo rasmi juu ya mpango wa kumsajilii Martinez baada ya kumuuza kipa wa Cameroon, Andre Onana, mwenye umri wa miaka 29. (Football Insider)

Beki wa Liverpool mwenye umri wa miaka 22 na raia wa England, Jarell Quansah, atafanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Bayer Leverkusen siku ya Jumatatu kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 35 kwenda klabu hiyo ya Ujerumani. (Fabrizio Romano)

Liverpool wako karibu kukamilisha dili usajili wa beki wa kati wa Crystal Palace, Marc Guehi, raia wa England mwenye umri wa miaka 24. (Mirror)

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Marc Guehi

Darwin Nunez yuko tayari kujiunga na Napoli msimu huu wa joto, lakini klabu hiyo ya Italia haiko tayari kutoa pauni milioni 70 ambayo Liverpool wanaitaka kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji huyo kutoka Uruguay mwenye umri wa miaka 26. (Mirror)

Skip Iliyosomwa zaidi and

End of Iliyosomwa zaidi

Manchester United huenda wakalazimika kuwalipa wachezaji wao ili waondoke klabuni msimu huu wa joto kutokana na mikataba yao ya muda mrefu na yenye gharama kubwa, huku mshambuliaji wa England Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 27, na winga wa Argentina Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 20, wakiwa miongoni mwa wanaotakiwa kuuzwa. (Telegraph)

Sunderland wamekubaliana na Strasbourg ada ya uhamisho ya rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 30 kwa kiungo wa Senegal mwenye umri wa miaka 21, Habib Diarra. (Guardian)

Nottingham Forest wamewasilisha ofa ya pauni milioni 5 kwa ajili ya beki wa pembeni wa Real Mallorca, Pablo Maffeo, raia wa Uhispania mwenye umri wa miaka 27. (El Chiringuito)

Marcus Rashford

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Marcus Rashford
Hauhitaji Whatsapp

Mwisho wa Whatsapp

Newcastle na Burnley bado hawajakubaliana juu ya thamani ya kipa James Trafford, ambapo Newcastle wamewasilisha ofa ya awali ya pauni milioni 25 kwa kipa huyo wa England mwenye umri wa miaka 22 lakini imekataliwa. (Sky Sports)

Crystal Palace wako tayari kushindana na Newcastle, Liverpool na Tottenham katika harakati za kumsajili winga wa Southampton, Tyler Dibling, raia wa England mwenye umri wa miaka 19 msimu huu wa joto. (Football Insider)

Nico Williams ameieleza Barcelona kuwa anataka kujiunga nao kutoka Athletic Bilbao, lakini winga huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22 ameitaka klabu hiyo kuhakikisha kwamba atasajiliwa rasmi ili aweze kucheza, jambo ambalo linaweza kuilazimu Barca kuuza baadhi ya wachezaji ili kutimiza masharti ya kifedha ya La Liga. (Marca - in Spanish)

Al-Nassr tayari wamefikia makubaliano ya kumpeleka mshambuliaji wa Colombia, Jhon Duran, mwenye umri wa miaka 21, kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce. (Foot Mercato)