
Liverpool wamejiunga na klabu za Manchester United na Arsenal katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Sporting mwenye umri wa miaka 27, raia wa Sweden, Viktor Gyokeres. (Correio da Manha)
Chelsea wako karibu kukamilisha usajili wa winga wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 21, Jamie Gittens, 20, huku klabu hiyo ya Bundesliga iking'ang'ania dau la pauni milioni 50. (ESPN)
Manchester United huenda wakakubali ofa ya takriban pauni milioni 45 ili kuhakikisha mauzo ya haraka ya winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 20, Alejandro Garnacho. (Star)

Newcastle wanawafuatilia wachezaji wawili, winga wa PSV Eindhoven na Ubelgiji, Johan Bakayoko, 22, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Karim Adeyemi, 23, ili kuwa mbadala iwapo watashindwa kumnasa winga wa Nottingham Forest na Sweden, Anthony Elanga, 23. (Teamtalk)
Manchester United wanapambana kumuuza beki wa kushoto raia wa Uholanzi, Tyrell Malacia, 25, ambaye alisaidia PSV Eindhoven kushinda taji la Eredivisie akiwa kwa mkopo msimu uliopita. (Athletic)
End of Iliyosomwa zaidi
Sunderland wamefanya mazungumzo na Nice kuhusiana na mpango wa kumnunua kipa wa Poland mwenye umri wa miaka 25, Marcin Bulka. (Fabrizio Romano)
Everton wameanza mazungumzo na klabu ya La Liga, Villarreal, kuhusu usajili wa mshambuliaji mfaransa mwenye umri wa miaka 22, Thierno Barry na huenda wakalipa pauni milioni 34 iliyoko katika mkataba wake. (ESPN)

Manchester City wamekataa ofa ya pauni milioni 6.5 kutoka Hoffenheim kwa ajili ya beki wao wa timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 21, Callum Doyle, 21. (Mail)
Everton bado wana matumaini ya kumsajili Kenny Tete kwa uhamisho wa bure licha ya ripoti kuwa Fulham wamempatia beki huyo wa kulia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 29 mkataba mpya. (Independent)
Benfica bado hawajapokea ofa kutoka Real Madrid kufuatia miamba hiyo ya La Liga kuhuhusishwa na beki wa kushoto raia wa Hispania, Alvaro Carreras, 22, ambaye amejiunga na klabu hiyo ya Lisbon msimu uliopita akitokea Manchester United. (Marca)